Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Kitulo

Watanzania wamehamasishwa kujenga tabia ya kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo nchini vikiwamo vya Hifadhi ya Taifa Kitulo.

Hifadhi hiyo iliyopo kwenye mikoa mwili; Njombe katika Wilaya ya Makete na Mkoa wa Mbeya katika Wilaya za Rungwe na Mbeya vijijini, inavutia kwa maporomoko ya maji, uoto wa asili na wanyama kama swala.


Mhifadhi Mkuu wa Kanda ya Kusini, Jonathan Kaihura anaitaja kuwa na vivutio saba vya kusitajabisha ukiachilia madhari yake nzuri na ya kipekee katika ukanda huo.

“Pamekuwa na dhana ya kwamba wanaopaswa kutembelea hifadhi na kufanya utalii ni wageni kutoka nje ya Tanzania, dhana hii si sawa. Nivema Watanzania tujenge utamaduni wa kufanya utalii kwenye hifadhi zetu,” amesema Kaihura mbele ya waandishi wa habari waliotelembelea hifadhi hiyo.

Januari 22 , 2024 timu ya wanahabari ilifika makate na kupata wasaa wa kuzungumza na Kaihura ambapo katika mambo mbalimbali alieleza kuwa imenzishwa mwaka 2005 ikiwa na upekee wa kuwa hifadhi inayopatikana nyanda za juu kusini.
Hifadhi ya Kitulo ina uoto wa asili na inayo pia maporomoko yaliyopo kwenye msitu ya mto Nhumbe.

“Kitulo imebarikiwa mno, haya maji yanayotiririka musimu wote kwenye chanzo chake pamepewa jina Mwakitelima, hili jina ni aliyekuwa Mhifadhi mkuu wa kwanza katika hifadhi hii,” amesema huku akisisitiza Watanzania kutembelea vivutio hivyo.


Gharama za kuingia katika hifadhi hiyo kwa mujibu wa Kaihura ni kidogo na rafiki ambapo kwa upande wa maradhi anasema kulala kwenye nyumba zilizopo hifadhini kwa siku ni sh 29,000 huku huduma ya chakula na vinywaji nayo ikiwa si ya kutisha.

“Kwa wale wanaopenda kuona wanyama hapa kwenye hifadhi yetu pia wapo. Mgeni akifika atawaona swala na wanyama wengine,” amesema.

Kwa upande mwingine amesema hifadhi hiyo ina aina 45 za maua na mimea ya aina mbalimbali hivyo kuwa fursa adhimu kwa Watanzania kushuhudia uzuri wa taifa ambalo Rais Samia Suluhu Hassan kwa moyo wa dhati ameamua kulitangaza vivutio vyake duniani kote.

Hifadhi ya Taifa ya kitulo ipo umbali wa mita 2900 kutoka usawa wa bahari na inazunguka katika mikoa miwili: Mkoa wa Njombe ambapo inapatikana Wilaya ya Makete na mkoa wa mbeya katika wilaya ya mbeya vijiji na wilaya ya Rungwe.