Mamowari ya Marekani Carl Vinson inafanya ziara ya kihistoria nchini Vietnam kwa mara ya kwanza kwa meli ya aina hiyo kuzuru Vietnam tangu vita kumazilika.
Manowari hiyo inayotumia nishati ya nyuklia itatia nanga katika bandari wa Danang ambapo wanajeshi wa Marekai walitua kwanza wakati wa vita.
Hii inamaana ya kuonyesha ushirikiano wa kijeshi kati ya nchi hizo.
Lakini wadadisi wanasema kuwa hii inatuma ujumbe kwa China wakati inaendelea kujiimarisha maeneo ya kusini mwa bahari ya China.
China kwa sasa ndio taifa lenye nguvu zaidi eneo hilo na pia mshirika mkubwa wa kibishara wa Vietnam.
Kwa hivyo utawala wa komunisti wa vietnam unachukua tahadhari kuzuia hatua ambazo zinaweza kuvuruga uhusiano na jirani wake China.
China inadai kumiliki karibu eneo lote la bahari ya Kusini mwa China vikiwemo visiwa ambavyo pia vinadaiwa na mataifa mengine.
Mara kwa mara Marekani imesema kuwa haiegemei upande wowote kwenye mzozo wa kusini mwa bahari ya China lakini jeshi la wanamaji wa Marekani limekuwa likiendesha doria eneo hilo ishara ya kuonyseha ubabe wa kijeshi dhidi ya China.
Manowari ya USS Carl Vinsion imefanya safari nyingi kwenye eneo hilo wakati wa miongo kadhaa ya huduma zake na mara ya mwisho ilikuwa eneo hilo ilikuwa siku chache zilizopita.
Vita vya Vietnam ambyo Vietnam huviita Vita ya Mareknia, vilikuwa vibaya. Serikali ya Vietnam inakadiria kuwa mamilioni ya watu raia na wapiganaji wa Komunisti waliuawa. Zaidi ya wanajeshi 58,000 wa Marekani nao waliuawa au kutoweka.