Akemea upotoshwaji wa masuala nyeti ya kitaifa

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bara, Philip Mangula, amesema ni kawaida kwa kiongozi mahiri kuanzisha au kukamilisha miradi ya maendeleo hata iliyo nje ya ilani ya uchaguzi ya chama chake kwa kuzingatia kuwa ilikwisha kuwapo katika mipango ya jumla ya kitaifa.

Mangula ameyasema hayo katika mahojiano maalumu na Gazeti la JAMHURI mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuwapo sintofahamu kuhusu kauli aliyoitoa hivi karibuni kwamba kilichoko kwenye ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 ni ujenzi wa gati, si bandari ya Bagamoyo.

Amesema pamoja na kwamba Ilani ya mwaka2020katikakifungucha59(b) (i) inazungumzia ujenzi wa gati katika bandari ya Bagamoyo, lakini Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye ndiye msimamizi mkuu wa utekelezaji wa ilani hiyo, anayo haki ya kujiongeza kwa kwenda mbali zaidi kwa kuamua kuanzisha mradi wa bandari badalayagati. “Hilisijambolaajabuhata kidogo, lilishafanywa na watangulizi wake. Mtakumbuka hata ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma uliofanywa na Rais wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Jakaya Kikwete, baada ya CCM kuiuzia serikali majengo yale,” amedokeza Mangula.

Anaongeza zaidi: “Kwa kujali masilahi ya taifa na kiu ya kuleta maendeleo katika sekta ya elimu kama ambavyo ilani zote za CCM zimekuwa zikisisitiza na kutoa miongozo, Mheshimiwa Kikwete alikijenga chuo kikuu cha mfano kwa Tanzania na Afrika; hivyo Ilani ya mwaka 2015 kwenye kurasa za 90 na 93 ikataja mafanikio ya chuo hicho katika kuandaa walimu.”

Anasisitiza kuwa ilani ni mwongozo na ahadi za chama kwa wapigakura na Watanzania inayopaswa kunadiwa na wagombea ikizingatia mahitaji ya nchi ya wakati huo na uamuzi wa kimkakati wa miaka ya nyuma; na akashangaa inakuwaje mbunge wa CCM kutokulijua hili.

Mangula ametoa mfano wa uamuzi wa chama wa kuhamishia makao makuu ya nchi Dodoma akisema: “Dodoma tumesema sana tangu tulipoamua mwaka 1973 kwamba ndiyo makao makuu ya nchi. Kila mwaka tulipotaka kuhamia kikwazo kikawa fedha na pengine dhamira. Lakini akaja Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli
na Makamu wake wa Rais, Mama Samia, wakasema muda wa kuhamia Dodoma ni huu wa Awamu ya Tano.”

Mangula anasisitiza kwamba hata ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme kwa Nguvu za Maji la Julius Nyerere (JNHEP) unafuata maelekezo ya Ilani ya mwaka 2015 katika ukurasa wa 74 kuhusu kuongeza uzalishaji wa umeme kulingana na Sera ya Nishati ya Taifa. “Hayandiyomamboyamaendeleo kwamba yule mliyemkabidhi ilani anaweza kuitekeleza hadi akaweka ya nyongeza, kwa sababu shida ya Watanzania ni kuona wanapata maendeleo,” anasema Mangula huku akikumbushia kwamba hata mradi wa JNHEP ulitokana na mipango ya miaka ya 1970 kwenye Awamu ya Kwanza.

Mangula anataja masuala mengine kama ufufuaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) lililoanzishwa mwaka 1977 ambao ulikuwa ukifanywa na marais wa awamu za tatu na nne na baadaye kufanikiwa kwenye Awamu ya Tano. Mangula anaonyesha ukurasa wa 71 wa Ilani ya mwaka 2015 unaotaja uimairishaji wa huduma za ATCL kwa kuongeza uwekezaji na hali kadhalika ukurasa wa 2 wa Ilani ya mwaka 2020 unaotamka kwamba ATCL itafufuliwa kwa kununua ndege 11.

Anatoa mifano zaidi kwamba katika sura ya tatu ya Ilani ya mwaka 2015 kuna mwongozo wa ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya usafiri na usafirishaji na ndiyo uliokuwa mwongozo wa ujenzi wa barabara, madaraja, barabara za juu, vivuko, bandarinarelihatimayekuwezeshadaraja la Kigongo-Busisi kuanza kujengwa chini
ya Awamu ya Tano kama ilivyo kwa reli ya kisasa (SGR) na miradi mingine.

“Sura ya pili ya Ilani ya mwaka 2020 kwenye ukurasa wa 77 inasisitiza kuhusu ukamilishaji wa madaraja saba likiwamo hili la Kigongo-Busisi (Mwanza),” anasema Mangula huku akionyesha orodha ndefu ya miradi ya miundombinu katika ilani hiyo.

Ameongeza: “Nashangaa upotoshaji uliofanywa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwa sababu kila mtu anajua hata kukitokea leo mkorofi mmoja akavamia nchi yetu Amiri Jeshi Mkuu hawezi kusema huyo adui asipigwe kwa sababu hilo halikuandikwa kwenye ilani,” na kusisitiza zaidi kwamba ilani ni mwongozo unaostahili kuwa na nyongeza kila inapobidi.

Mwanasiasa huyo mkongwe ametoa mwito kwa wana CCM na Watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais Samia katika kutekeleza mambo makubwa kwa manufaa ya nchi huku akisema hata mpango wa kuwatengea maeneo wamachinga umo katika Ilani ya mwaka 2020.

“Ninachokumbuka ni kuwa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ambao pia ulitajwa kwenye Ilani ya mwaka 2015 haukufutwa na Mheshimiwa Magufuli, bali alipenda mikataba iwe na masilahi kwa taifa ili kuona wawekezaji wanapata na sisi Watanzania tunapata. Naamini ndiyo kazi itakayofanywa na Awamu ya Sita kwa kurejea katika mazungumzo ili kuhakikisha taifa linapata masilahi yake na inapowezekana inajengwa bandari badala ya gati,” anamaliza Mangula.

Ameulizwa kuhusu minong’ono kuwa ufufuajiwamazungumzoyamradiwa bandari ya Bagamoyo unaweza ukatoa fursa ya ufisadi katika Awamu ya Sita, Mangula amehamaki na kusema: “Wote mmesikia juu ya hatua kali alizochukua Mheshimiwa Rais juu ya tuhuma za ufisadi Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL). Watu waache upotoshaji na hisia, badala yake wamuunge mkono Mheshimiwa Samia, kwani anaonyesha ujasiri na dhamira ya dhati ya kuijenga Tanzania.”