Kufuatia video fupi kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikionyesha kutokea kwa ajali ya ndege iliyodaiwa kuzama katika Ziwa Victoria leo Februari 23, 2023 Mkrugenzi wa Mamalaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) Mussa Mbura amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa hakuna ajali bali ni mazoezi ya utayari

kizungumza na moja wapo ya vyombo vya habarai hapa nchini Mkurugenzi huyo amesema hakuna ajali ya ndege leo kwenye Ziwa Victoria Jijini Mwanza bali kilichofanyika ni mazoezi ya utayari, imeripotiwa

“Haya ni mazoezi ya kujiweka tayari ambayo tumeendelea kuyafanya, kama Mamlaka za Viwanja vya Ndege miongozo inatutaka tuwe tuanafanya mazoezi ya mara kwa mara kuhakikisha watu wetu wapo tayari pale inapotokea tatizo kila mtu kwenye eneo lake awe tayari” Mussa amekiambia chombo hicho

Aidha, Mbura amesema kuwa katika Viwanja takribani 58 vilivyopo chini inatakiwa mazoezi yawe yanafanyika katika viwanja vyote na huo ni muendelezo tu na hakuna ajali halisi.

Mazoezi haya yamefanyika ikiwa ni siku kumi zimepita tangu isambae taarifa kama hii Februari, 13 2023 katika mitandao ya kijamii ikidai kutokea kwa ajali ya ndege ambapo iliripoti watu kumi kufariki dunia na kadhaa kujeruhiwa katika uwanja wa ndege uliopo Kahama, hata hivyo taarifa hiyo baadaye ilikanushwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mboni Mhita kuwa haikuwa ajali bali yalikuwa mafunzo ya utayari.