Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Arusha
Kambi ya Madaktari bingwa Imeanza kuhudumia wananchi wa Mkoa wa Arusha kwenye Kliniki maalum iliyoanza leo Juni 24, 2024 ikitarajiwa kufanyika kwa siku saba Mfululizo kwenye Viwanja vya michezo vya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Hatua hii ni utekelezaji wa vitendo wa azma ya Serikali ya awamu ya sita ya kulinda nguvu kazi ya Taifa kwa kuwapatia wananchi huduma bora za afya hususani katika nyanja za uchunguzi wa magonjwa, elimu ya afya kwa Umma na kuimarisha huduma za tiba na kinga kwa jamii.
Lengo la Kambi ya Matibabu haya ni kuwapa wananchi fursa ya kupata elimu ya afya, vipimo vya magonjwa mbalimbali na ushauri wa kitaalam ili kupata huduma stahiki za tiba na kinga ambapo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha inashirikiana na sekta binafsi, Hospitali na Taasisi mbalimbali za Matibabu.
Kaulimbiu ya Kambi hii ya madaktari bingwa inasema “Afya yako mtaji wako, kazi yetu ni kukupatia huduma bora”