Hotuba ya Rais Mwalimu Julius Nyerere kwenye Sherehe ya Kufungua Kiwanda cha Nguo Ubungo Dar es Salaam Julai 6, 1968

Waheshimiwa, Mabibi na  Mabwana,
Kukusanyika kwetu hapa leo, ili kukifungua kiwanda hiki cha nguo ni jambo la furaha kuu na la kujivunia. Sherehe  hii ni mfano mwnigine wa hatua tunayopiga katika lengo letu la kujitegemea, na vilevile inaonyesha jinsi tulivyo tayari kupokea misaada inayotufaa kutoka katika nchi zingine. Kwa kweli kujengwa  kwa kiwanda hiki kunadhihirisha kwamba juhudi yetu ya kujitegemea haina shabaha ya kuwachukia watu wa nchi nyingine, wala ya kukataa  kabisa misaada wanayotaka kutupa, ikiwa misaada hiyo hatimaye itatuwezesha kujitegemea zaidi.  Za misaada inayotufaa maana yeke ni misaada itakayotuwezesha kujitegemea zaidi hapo baadaye.
Kiwanda hiki cha nguo ni cha Tanzania. Ni mali yetu; na tuna wajibu wa kukiangalia. Lakini kiwanda hiki kipo leo kwa sababu ya msaada tuliopokea kutoka Jamhuri ya Watu wa China. Watu wa nchi hiyo wametusadia kwa kutupa mkopo mkubwa, na watalaamu waliokijenga kiwanda. Mafundi wa Kichina wametusadia kukijenga kiwanda hiki, na wanafunza kwa bidii Watanzania watakaoendesha kiwanda baada ya wao kuondoka. Napenda kusema kwamba kwa moyo na juhudi yao ya kufanya kazi ngumu, wametupa sote sisi mfano mzuri wa kuiga.
Kwa hiyo, kwa niaba ya Watanzania wote napenda kutoa shukurani nyingi kwa sababu ya msaada huu wenye manufaa sana. Naamini kwamba wewe, Bwana Balozi utaupeleka ujumbe huo wa   shukurani kwa Serikali na watu wote wa nchi yako. Tunapeleka salamu zetu pamoja na uthibitisho kwamba vema kiwanda hiki ambacho nchi yako imetusadia kukipata.
Kiwanda hiki cha nguo kimetuundia nafasi gani? Kinawezaje kutusadia katika shabaha yetu ya kujitegemea, ambapo karibu fedha yote ilitumiwa kukijenga ni fedha ya Wachina, na kimejengwa kwa msaada wa Mfundi wa Kichina?
Kiwanda hiki cha nguo ni chombo kipya; ni chombo kitatakachoongeza idadi ya vitu tutavyootengeza. Kama mkulima anavyoweza kuongeza ukubwa wa shamba lake akitumia plau badala ya kutegemea jembe, vivyo hivyo tukitumia kiwanda hiki tunaweza kuongeza kiasi cha mali itakayozaliwa katika Tanzania. Lakini ikiwa Tanzania inataka kupata manufaa kutokana na kuwapo kiwanda hiki, basi kiwanda hiki lazima kitumiwe na kuangaliwa vema, kama vilevile ambayo plau la mkulima lazima litumiwe na kutunzwa kabla ya mkulima kupata mavuno yake. Wachina wametusadia  kuunda chombo hiki. Ni juu yetu sasa kukitumia kwa busara.
Hapo zamani wakulima walilima pamba, na tukasafirisha pamba hiyo, pamoja na mbegu zake, kuuza katika nchi zingine. Watu  wa nchi zingine waliigeuza pamba ikwa nguo; na sisi tukanunua  tena nguo hizo. Kwa kweli tulivyokuwa tunafanya ni kulipa mishahara na faida, kwa watu katika nchi zingine kwa ajili ya kufuma pamba yetu. Kuwako kwa kiwanda hiki, na viwanda vingine vinavyotengeza nguo katika Tanzania, maana yake ni kwamba hatutalazimika kufanya hivyo tena. Kabla ya  mwaka huu kwisha  tutakuwa tunasokota pamba, tunatengeza kanga, vitenge na nguo za aina nyingine, kutokana na kiasi chochote cha pamba kitakachotosha kuwavika watu wote wa Tanzania.
Ndiyo kusema kuwa kuwapo kwa kiwanda hiki na viwanda vingine vipya vya nguo kutaifanya Tanzania isitegemee nchi nyingine yoyete kupata nguo za pamba. Badala ya kuwalipa mshahara wasokotaji pamba na wafumaji wa Ulaya, sasa tutakuwa tunawalipa wa Tanzania. Badala ya kuachia kampuni za kigeni zipate faida kutoka na pamba wanayonunua kwetu, na kutuuzia tena baada ya kufuma, sasa kiwanda hiki; faida yote itakayopatikana itakuwa faida ya umma, maana kiwanda hiki ni mali ya umma. Lakini mtu asidhani kwamba sasa  pamba yote inayolimwa Tanzania itakuwa katika viwanda vyetu wenyewe. Hata wakati ambapo viwanda vyetu vya nguo vitakapokamilika, pamba itakayotumiwa katika viwanda vyote vya Tanzania itakuwa 10% tu ya pamba tunayolima. Pamba iliyobaki haina budi iuuzwe katika nchi za ngambo, kama ilivyo sasa, na bado bei atakayopokea mkulima itategemea bei za masoko  ya dunia, ambayo hatuna mamlaka nayo. Lazima shabaha yetu ya hatimaye iwe kutengenza nguo nzuri zenye kupendeza, na kwa bei ambayo wananchi wataimudu. Kiwanda cha Tanzania kisichoweza kufanya hivyo hakina manufaa kwa wananchi wa Tanzania. Maana yake neno hilo ni kwamba lazima uongozi uwe mzuri, na wafanyakazi wawe waangalifu, wenye bidii, na hima ya kazi. Kila mtu anayefanya wanunuzi wa bidhaa zake, au aliye na kazi ya kusafirisha bidhaa, ama kuingia kutoka katika kiwanda hiki, ana wajibu kwa Tanzania.
Wafanyakazi wa kiwandani lazima wafanye kazi kwa bidii wakati wote wakiwamo katika zamu yao ya kazi; lazima wawahi kazini, na waondoke baada ya kazi yao ya kila siku kumalizika siyo kabla. Lazima waingalie mitambo iliyomo maana mitambo hiyo ni mali yetu. Kama mitambo hiyo ikiharibiwa kwa uzembe au upuuzi wa mtu mmoja, basi watu wa Tanzania watakuwa wamepungukiwa fedha za kununulia vitu vingine,  maana fedha tutaitumia kununua mtambo mpya, ama kutengeneza ule ulioharibika. Mafundi hawana budi kuhakikisha kwamba makosa hayatokei wakati wawa kufuma, maana hakuna mtu anayetaka kununua nguo mbovu. Lazima wajivunie kufanya kazi katika kiwanda hiki, ambacho licha ya sifa zingine, ni kiwanda cha kana katika Afrika Mashariki kinachoweza kutia ulembo nguo za pamba. Na kwa kazi yao, wafanyakazi hao wanaweza kutegemea kupata heshima, mshahara mzuri, na hali nzuri za kazi.
Lakini sina budi kusisitiza kwamba heshima ambayo mfanyabiashara anaweza akatarajia maana yake siyo kukataa kufuta utaratibu, au ulegevu kazini. Watu wanapofanya kazi pamoja, utii ni kitu cha lazima. Usikivu uwe nao kila mtu; wafanyakazi wenyewe watambue kwamba kama wanataka kuongeza bidhaa zifikie kima chake cha mwisho, basi vitendo aina  kadha havifai. Lakini ikiwa wafanyakazi hawatambui hivyo kwa nafasi zao, basi lazima utaratibu  huo uwekwe na wakuu wa kazi. Inaelekea kwamba watu wengine katika nchi hii wanalisoma Azimio la Arusha kwa kutilia mkazo starehe tupu. Eti Azimio linasema kwamba wanaweza kulegea kazini, na wanyapara wao wasiwaulize. Hili si kweli. Azimio la Arusha linataka utii zaidi si utovu wa adabu. Azimio halitaki mfanyakazi anayonywe, linataka  matunda ya jasho letu yafaidiwe na wale wanaofanya kazi. Lakini hilo maana yake ni kwamba lazima vile wakubali na wajibu. Watu kumi wakikusanyika kuinua gogo zito,  lazima wote watoe nguvu zao zote pamoja, na kwa wakati mmoja.
Kama mmoja wa wale kumi akichelewa, au akiinua kwa ulegevu, basi moja katika  katika mambo haya kuliko walivyopaswa (na kama hivyo ndiyo ujira wakuinua gogo ungepaswa kugawiwa kwa watu tisa sio kumi); ama gogo lile halitainuka kabisa (na hapo juhudi za wale tisa zitakuwa zimepotea bure) kufuta utaratibu wa kazi ni jambo muhimu, na kutika jambo hilo pia mafundi wa Kichina wametuonyesha mfano mzuri. Lakini  kazi ngumu, nzuri au yenye utaratibu katika kiwanda pekee yake haina maana.