Malawi imetangaza kuwa janga la kitaifa hali ya ukame inayokumba sehemu kubwa ya nchi hiyo.
Tangazo hilo linakuja chini ya mwezi mmoja baada ya taifa jirani la Zambia kuchukua hatua kama hiyo.
Rais wa Malawi Lazarus Chakwera ameomba zaidi ya dola milioni 200 kama msaada wa kibinadamu.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani limesema mataifa kadhaa ya kusini mwa Afrika nakabiliwa na tishio la baa la njaa kwa sababu ya athari za hali ya hewa ya El Nino.