Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia,Dar es Salaam

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kuvuka lengo na kukusanya
sh.trioni 7.79 , kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha Julai hadi Septemba 2024.

Makusanyo hayo yalionyesha mwezi Julai hadi Septemba 2024 asilimia 104.9 wakati lengo lilikuwa 7.42

Azungumza na waandishi wa habari Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania, Yusuf Mwenda amesema makusanyo katika mwezi Julai 2023/2024
1.94 na 2024/2025 lengo lilikuwa kukusanya 2.25 na makusanyo 2.35 ufanisi asilimia 104.5 ukuaji asilimia 21.1 ,Agosti 2023/2024
ukusanyaji 2.01.

“Mwaka 2024/2025 lengo lilikuwa 2.30, makusanyo yalikuwa 2.42 ufanisi
105.5% ukuaji 20.4 % , Septemba 2023/2024 makusanyo yalikuwa 2.62 Septemba 2024/2025 lengo lilikuwa 2.88 makusanyo yalikuwa 3.02 ufanisi 104.8 na ukuaji 15.0 asilimia.

Jumla ya makusanyo mwaka 2023/2024 yalikuwa 6.57, mwaka 2024/2025
lengo lilikuwa 7.42 makusanyo yalukwa 7.79 ufanisi 104.9 asilimia na ukuaji asilikia 18.4.

Makusanyo haya ya mwaka 2023/2024 ni ya kiwango cha juu kabisa, ambacho akija wahi kufikiwa na TRA kwa miezi ya julai na septemba ya mwaka wa fedha ambayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 77.4
ikilinganishwa na makusanyo ya kipindi kama hicho katika mwaka 2020/2021

Mwaka 2024/2025 lengo lilikuwa 7.42 makusanyo yalikuwa 7.79 ufanisi asilimia 105.0 ukuaji asilimia 18.4 na mwaka 2023/2024 lengo lilikuwa 6.75 makusanyo yalikuwa 6.57 ufanisi aslimia 97.5 ukuaji aslimia 11.0.

Mwaka 2022/2023 lengo lilikuwa 5.98 makusanyo 5.92 ufanisi asilimia 99.1 ukuaji asilimia 14.6,mwaka 2021/2022 lengo lilikuwa 5.46 makusanyo yalikuwa 5.17 ufanisi ilikuwa asilimia 94.6 ukuaji asilimia 17 .9.

Mwaka 2020/2021 lengo lilikuwa 5.06 makusanyo 4.39 ufanisi asilimia
86.6, pia katika kipindi cha mwezi Septemba 2024/2025 TRA imekusanya kiasi cha Sh.Trilioni 3.02 sawa na ufanisi wa asilimia 105 ya lengo la kukusanya sh. Trilioni 2.88 ni makusanyo ya kiwango cha juu cha ukuaji
wa asilimia 77.6 kuweza kukusanywa na TRA katika mwezi septemba ndani ya kipindi cha miaka mitano tangu mwaka 2020/2021”Amesema .

Mwenda amesema ufanisi wa makusanyo uliyofikiwa na TRA kwa miezi ya Julai hadi septemba, ni kiashiria chanya katika kuhakikisha kuwa lengo la makusanyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 la sh. trioni 30.04 linafikiwa.

Amesema ufanisi huo, umechangiwa na kuendelea kutekeleza kwa vitendo,
maagizo na maelekezo ya mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuendelea kuhamasisha ulipaji kodi wa hiari

‘”Tumeshirikiana na walipa kodi, kwa kuwasikiliza na kutatua changamoto zao ili kuleta chachu ya kukua kwa uchumi na ongezeko la uwekezaji kutokana na sera nzuri za awamu ya sita.

TRA inapenda kukuza ushirikianano na mahusiano kati ya walipa kodi wote nchini , kuendelea kulipa kodi kwa hiari na tuna endelea kupokea maoni kutoka kwa viongozi wa vyama vya wafanyabishara wote nchini.

Kuendelea kuweka kipaumbele katika utoaji wa huduma bora kwa walipa kodi, zinazozingatia mahitaji ikiwemo kuwahudumia walipa kodi (Jmosi na
Jpili )kupitia ofisi zote za TRA nchini pamoja na kuwatembelea katika sehemu zao za biashara ili kuwasilikiliza na kutatua changamoto za kikodi walizo nazo kwa wakati” amesema.

Amesema utendaji mzuri katika kazi na kujituma kwa watumishi, pamoja
na taasisi zingine wanaoshirikiana nao katika kazi ya ukusanyaji wa mapato kuendelea kuboresha mahusiano ambapo siku ya alhamisi kuwa maalumu kwa ajili ya kuwasiliza walipa kodi kupitia ofisi zote za
TRA.

“Kuongezeka kwa usimamizi wa wafanyabishara kwa kukemea vitendo vya
uvunjifu wa maadili, ikiwemo kukemea vikali vitendo vya rushwa na kuchukua hatua kwa wanaopatikana na kuhusika na vitendo hivyo sambamba na kuchukua hatua za haraka za kutatua changamoto za walipa kodi
wanazo wasilisha moja kwa moja kwenye ofisi ya kamishina mkuu kupitia TRA SIKIKA APP iliyozinduliwa mwezi agusti 2024 .

Kuendelea kuimarisha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji, kwa kuhakikisha marejesho ya madai ya kodi yanafanyika kwa wakati ili kufanikisha fedha hizo kurejeshwa kwenye mzunguko shughuli za kiuchumi
nchini .

Kuendelea kutekeleza kwa vitendo maelezo yaliyotolewa na serikali, ikiwemo la utengenezaji wa mfumo wa kurahisisha ugomboaji wa mizigo inayoingia kwa utaratibu kwa ufungishaji wa mizigo (Consolidation ).

Kuendelea kuboesha mazingira ya ufanyaji biashara nchini, kwa kusimamia kikamilifu bidhaa nane ambazo zimewekewa bei elekezi ambazo ni (Vitenge,Mashati,Nguo zingine,Vipodozi ,Vito vya thamani ,Nguo za
ndani ,leso na Vesti )

Kufuatilia kwa ukaribu hali ya ufanyaji biashara nchini ,kwa kusimamia
kikamilifu uzalishaji wa viwandani pamoja na matumizi ya mashine ya EFD nchini “amesema.

Amedai kuendelea kusimamia utawala wa sheria za kodi kwa haki ,bila kupendelea wala kumwone mlipa kodi yeyote ili kuweka mazingira ya bishara yaliyo sawa.

“Kwa sasa TRA inaendele kuimarisha mahusiano na walipa kodi, kupitia
utoaji wa huduma bora pamoja , kampeni za elimu kwa mlipa kodi na kuimarisha usimamizi wa utoaji wa risiti za kielectroniki EFD”Amesema.

Amesema kuendelea na ujenzi na uimarishaji wa mifumo ya kodi za ndani na forodha (IDRAS na TANCIS), inayosomana na mifumo mingine nchini kwa kusimamia na kuimarisha misingi ya mfumo mzuri wa kodi ikiwemo haki usawa katika utozaji kodi (no favouritism or victimization) ili kuweka mazingira ya biashara yaliyo sawa.

‘’Kushirikiana kwa kikamilifu na timu iliyoteuliwa na mheshimiwa Rais,
inayofanya mapitio ya mfumo wa kodi nchini ili kuleta maboresho akubwa katika mifumo ya kodi nchini na kuimarisha na kusimamia weledi (professionalism ) na huduma nzuri kwa walipa kodi ikiwemo watumishi
wetu wote kuvaa vitambulisho wanapotoa huduma

Kuimarisha vitengo vya ukaguzi na uchunguzi wa kodi ,ili kuzuia ukwepaji kodi za ndani na forodha na kuondoa upotevu wa mapato ya
Serikali na kuweka mazingira ya biashara yaliyo sawa kwa wafanyabishara wote

Amesema kwa sasa TRA imejipanga kuimarisha vitengo vyote na kupata
taarifa kwa wakati, ili wale wanaokwepa tuweze kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria

Aidha kamishana wa forodha Juma Bakari amesema , kodi mbalimbali zinazokusanywa ,zipo kwa mujibu wa sheria zinasimamia bidhaa zinazotoka na zinazo kwenda nje.

Bakari amesema kodi zinatozwa kwa kuzingatia viwango , vilivyopitishwana na mamlaka husika pia thamani ya mzigo inayopatikana kupitia nyaraka zenye taarifa sahihi za mzigo.

“Ni wajibu wa muingizaji bidhaa kutunza nyaraka sahihi za kuchukulia
bidhaa, lakini tuko kwenye mpango wa kuandaa mfumo wa utunzaji na
ulipaji kodi ambao utaondoa migongano kati ya wafanyabiashara na TRA .

Mifumo hii itaanza kufanya kazi ifikapo january 2025,ambapo wananchi
wajiandae hawatokuja tena ofisini bali mifumo ndio itafanya kazi zaidi
kwa kufanya makadirio sahihi”Amesema

Alfred Mregi kamishina wa kodi za ndani amesema ,Mfanyabishara ajue bidhaa zake zinazoingia na kutoka ili wanapokuja kukusanya kodi ziendane na uhalisia wa kumbukumbu zako.

Mregi amewakumbusha wafanyabishara na wananchi ,kulipa kodi kwa wakati na kuwasilisha Return ili kuepuka adhabu