Baadhi ya magari ya vyombo vya ulinzi na usalama ambayo yanaendelea kutengenezwa ambayo yalipelekwa yakiwa yameharibika kabisa
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akizungumza leo wilayani Mkuranga mkoani Pwani wakati alipoenda kukagua magari 11 ya vyombo vya ulinzi na usalama yanayotengenezwa na Kampuni ya Dar Coach.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akipewa maelezo leo na Mkurugenzi wa kampuni ya Dar Coach Manmeet Lal kuhusu hatua waliyofikia katika kufanya matengenezo ya magari 11 ya vyombo vya ulinzi na usalama
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikagua magari 11 ya vyombo vya ulinzi na usalama ambayo yanatengenezwa mabodi yake yaliyokuwa yameharibika.Matengenezo hayo yanafanywa na Kampuni ya Dar Coach Ltd
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikagua moja ya gari la Jeshi la Magereza leo inayofanyiwa matengenezo na Kampuni ya Dar Coach Ltd
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amepongeza hatua ambayo kampuni ya kutengeneza mabodi ya magari ya Dar Coach Ltd imefika y’all kutengeneza na kukarabati mabasi 11ya vyombo vya ulinzi na usalama.
Kati ya magari hayo magari matano yatakabidhiwa mwishoni mwa mwezi huu na mengine sita yatakabidhiwa.
Makonda amesema mmiliki wa kampuni hiyo amethibitisha uzalendo wake na mchango wake katika kusaidia Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam inayotaka kuona vyombo vya ulinzi na usalama wanakuwa na usafiri wa kisasa na uhakika ili kutekeleza majukumu yao.
Jumla ya Sh milioni 830 mmiliki wa kampuni hiyo anatumia katika kukarabati magari yote 11ambapo baadhi yamenfenezewa mabodi mapya kwani yalikuwa yameharibika sana.
Akizungumza leo baada ya kukagua magari hayo katika kampuni hiyo iliyopo Mwandege wilayani Mkuranga mkoani Pwani,Makonda amesema hatua ya ukarabati magari hayo umefikia pazuri na ameahidiwa kukabidhiwa baadhi ya magari hayo mwishoni mwa mwezi huu.
Amesema wakati matengenezo ya magari hayo unaendelea wapo watu kwenye mitandao ya kijamii wanalalamika kwanini yasinunuliwe magari mapya kwa madai gharama kubwa. “Wanaosema gharama ya kutengeneza magari ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ni kubwa wafahamu tu gharama za kutengeneza magari haya amejitolea mmiliki wa Kampuni ya Dar Coach Ltd,
“Ameamua kutoa mchango wake kupitia utalaam alionao wa kutengeneza mabodi ya magari ya majeshi yetu ambayo tumemletea. Ni mlipa kodi mzuri na kazi anayofanya ipo katika ubora unaokubalika.
“Hao wanaolalamikia ukubwa wa gharama pengine hawalipi hata kodi zaidi ya maneno tu. Huyu ametusaidia na tunathamin mchango wake kwetu,”amesema.
Ameomba kampuni nyingine kujenga utamaduni wa kujitolea kuisaidia Serikali na hakuna sababu ya kushurutishwa bali ni kuonesha uzalendo kwa kuunga mkono jitihada za Serikali ya kushughulikia kero za watanzania.
Makonda amesema ametoa ombi kwa kampuni hiyo kuhakikisha wanaweka na sehemu za kuchajia simu katika magari haul ili kuhakikisha mawasiliano ya simu yanakuwa muda wote kwa watakaoyatumia. “Lazima vyombo vya ulinzi na usalama wawe na magari mazuri. Kila mmoja akifanya kile ambacho anaweza kukifanya tutapiga hatua kubwa,”amesema Malinda.
Ameomba wananchi ambao wanataka kufanya matengenezo ya magari yao wapeleke katika kampuni hiyo kwani inatengeneza magari kwa kiwango cha juu cha ubora. Kwa upande wa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Manmeet Lal(Sunny)amesema gharama ya kutengeneza gari zote 11 ni Sh. milioni 830 na ndio mchango wao kwa Serikali na wataendelea kujitolea kadri watakavyoweza.
“Kampuni yetu iliona umuhimu wa kusaidia kufanya matengenezo ya magari haya na kwa gharama zetu wenyewe na tumeamua kusaidia kama sehemu ya kutoa mchango wetu kwa Serikali,”amesema Lal.
Akizungumzia ukarabati wa magari hayo Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema amefurahishwa na hatua anazochukua Mkuu wa mkoa Makonda za kuhakikisha vyomvo vya usafiri vilivyokuwa chakavu vinatengenezwa na kuwa imara.
Wakati huohuo Naibu Kamishna wa Magereza Augustino Mboje amesema matengeneza ya magari hayo kwa upande wao yatasaidia kuondoa changamoto ya usafiri hasa katika kusafirisha mahabusu.