Makamu wa Rais akiwasili Burundi kushiriki mkutano wa EAC
JamhuriComments Off on Makamu wa Rais akiwasili Burundi kushiriki mkutano wa EAC
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Melchoir Ndadaye uliopo Bujumbura nchini Burundi leo tarehe 31 Mei 2023. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa 21 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaofanyika nchini Burundi.