Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla ameweka jiwe la msingi kwenye  jengo la dharura kwenye Hospital ya Jeshi la Magereza Ukonga  ambayo inatoa huduma za afya kwa Jeshi la Magereza na  wananchi zaidi ya 900,000 wa Jimbo la Ukonga.

Akizungumzia wakati wa hafla hiyo, RC Makalla, leo Mei 4,2023 amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan  kwa kutoa zaidi ya Shilingi  Milioni 950 kwa ajili ya ujenzi huo ambapo Shilingi  Milioni 350  zimejenga majengo na  Milioni 600 zimehusika kwenye ununuzi wa vifaa tiba.

Aidha  CPA, Makalla  amepongeza Jeshi la Magereza kasi ya ujenzi ambapo mpaka sasa hospital imekamilika kwa asilimia 95  huku wakiomba kuongezewa Shilingi Milioni 118 Ili ikamilike kwa asilimia 100 ambapo mkuu wa mkoa amepokea kwa mikono miwili ombi hilo na ameahidi kulifanyia kazi.

Pamoja na hayo  RC Makalla amesema uwekezaji jiwe la msingi wa jengo hilo ni sehemu ya mwendelezo wa  maadhimisho ya Siku ya Muungano  ambapo pia
Ametoa wito kwa jeshi hilo kuendelea  kushirikiana na wananchi wa Ukonga katika masuala mbalimbali ya kijamii.