Sehemu ya tatu, mwandishi wa makala hii aliishia kwenye
maelezo ya namna Waafrika walivyozuiwa kunywa bia
katika Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam. Hatua hiyo
iliibua mgogoro mkubwa. Sehemu hii ya nne na ya mwisho,
mwandishi anaeleza umuhimu wa Waafrika kujiamulia
mambo yao wenyewe badala ya kutegemea Marekani na
Ulaya. Endelea…
Wazungu wote kwa ujumla wao hawakutuona sisi
Waafrika, watu weusi na wananchi wa nchi hii (Bara
la Afrika) kama tulikuwa watu (human beings).
Mtazamo ule ndio Baba wa Taifa aliita “jeuri ya
kikoloni”. Mwalimu aliita vile kwa sababu alisema
haya: –
“… Jeuri ya ukoloni ni jeuri ambayo inazidi jeuri
nyingine yoyote duniani. Ni jeuri ambayo waliyonayo
jeuri ile, wanakataa usawa wa watu wote.”
“Na kwa jeuri ile Wazungu waliamua tu kututawala
tupende, tusipende”.
Sasa Mwalimu anajenga hoja hivi; “Watawala wa

kikoloni walijifanya wao si watu bali walikuwa ni
miungu-watu.”
Akaendelea kutoa mifano namna hii, nanukuu:“…
kiongozi wa Wajerumani anaitwa Hitler, aliwachukia
sana Wayahudi …Hitler aliua Wayahudi milioni sita.
Na moja ya dhambi ya Wayahudi walihubiri USAWA
WA UBINADAMU…”
“…Hitler anasema UJINGA GANI HUU! BINADAMU
na mnyama hawezi kushindana katika mbio au
ngumi na hawa WEUSI wamewashinda hawa
(Wazungu) weupe kwa sababu wao (watu weusi) ni
WANYAMA, wanaweza sana mbio zaidi…”
Maneno haya Adolf Hitler aliyatamka katika Uwanja
wa Olympic kule Munich mwaka 1936, pale
alipoombwa kwenda kumvalisha medali ya dhahabu
Mnegro kutoka Marekani, Jesse Owens, aliyeshinda
mbio zile nafasi ya kwanza. Hitler alitoka na kususia
mashindano yale ambayo yeye alikuwa mgeni rasmi
siku ile.
Hakukomea pale, bali aliendelea kubwata maneno
ya maudhi wakati akitoka uwanjani pale. Baadhi ya
mabwato yake yalikuwa, namnukuu Mwalimu
Nyerere:
“…Hitler hakuishia hapo alikuwa anaamini watu
weupe hao wako weupe walio bora zaidi kuliko
weupe wengine na akadai kuwa magazeti ya
Kiyahudi yanapotosha badala ya kusema kwamba
watu weupe ni wa ajabu kweli…

v Hawa wanapotosha taifa letu la
wateule kwamba watu weusi ni sawa na

weupe. Badala ya kusema kwamba watu
weupe ni watu wa ajabu kweli, wanaweza
kumfundisha nusu nyani hawa sawa sawa
na binadamu…”
v Wanasema weusi fulani wanakwenda
vyuo vikuu na huko wanasoma na
wanahitimu wamepata shahada sawa
sawa na watu weupe au hata wamezidi.
(Tazama hotuba ya Mwalimu Nyerere ya
tarehe 09/12/1978, utajisomea mengi zaidi
ya haya.)

Nashauri kwa wale wasiokisoma kitabu cha Hitler
kinachoitwa “Mein Kampf by Adolf Hitler” (Sentry
Edition – The Riverside Press Cambrige) wapitie
kule Maktaba ya Taifa wakajisomee waonje kashfa
na maudhi ya Hitler kwa watu weusi na Wayahudi.
Hapo wasomi wa vyuo vikuu mnaona kebehi ya
Hitler kwa watu weusi?
Basi, jeuri ile ya Hitler imefanana sana na jeuri ya
makaburu wa Afrika Kusini enzi za mtawala
aliyeitwa Paul Krugger. Makaburu kwa ujumla wao
huwa hawakubali kwamba watu weusi wa Afrika
Kusini ni binadamu kama wao.
Kwa hali hiyo walileta sera ya ubaguzi wa rangi
(believed in subjection of black races) kati ya
Wazungu na watu weusi – Waafrika wenyeji.
Paul Krugger ndiye aliyetamka: “Blacks in South
Africa are drawers of water and wood cutters.”
Akimaanisha watu weusi hapa Afrika Kusini ni
vibarua wa kuteka maji na kuchanja kuni tu kwa ajili

ya Wazungu. Kama si jeuri ya kikoloni, matamshi ya
namna hii tuyaiteje? Ni kebehi na dharau na
udhalilishaji mkubwa kwa watu weusi.
Hata juzi juzi hapa tumesikia matamshi ya Rais wa
Marekani, Donald Trump (mwenye asili ya
Kijerumani) akimuita mfanyakazi wake wa ikulu
aliyetumbuliwa kutoka ikulu kwa majina “low life
people” na “dog”.
Huyu mama ana asili ya weusi – Mnegro. Matamshi
haya hayana tofauti na Hitler au Klugger, ni
udhalilishaji wa hali ya juu. Matendo na maneno
hayo ya Wazungu ndiyo Mwalimu aliyaita “jeuri ya
kikoloni.”
Sioni mantiki kwa hawa Wazungu na Wamarekani
kuja kuangalia uchaguzi wowote unaofanyika katika
nchi huru za Afrika. Haki hii amewapa nani?
Hebu fikirini matamshi ya Ubalozi wa Marekani
hapa