Amesema msiba utakuwa nyumbani kwa marehemu Mtaa wa Masuguru mjini Korogwe maarufu kama Mamba Club.
“Mazishi yatakuwa Julai 5, 2018 siku ya alhamisi saa 10 jioni kwenye makaburi ya kijiji cha Kwamndolwa. Ni baada ya kuswaliwa saa saba mchana kwenye Msikiti Mkuu wa Ijumaa mjini Korogwe” alisema Ngonyani.
“Majimarefu amefariki dunia Juni 2, 2018 saa tatu usiku kwenye chumba namba moja cha wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospitali ya Muhimbili, na alikuwa anasumbuliwa na Homa ya Mapafu kwa muda mrefu”,amesema.
“Pamoja na kuumwa arnimonia kali (homa ya mapafu), mara chache alikuwa anasumbuliwa na presha ya kushuka. Kabla ya hapo alikuwa anasumbuliwa na nyonga, na hiyo ilimfanya alazwe nchini India mwezi mmoja”, amesema Ngonyani ambaye yeye ndiyo aliyemlea Majimarefu.
Ngonyani amesema, Maji Marefu ameacha wake wawili Salma na Halia. Ni baada ya hivi karibuni kufiwa na mke mkubwa Bi. Mariam, huku watoto wakiwa 11, watoto wa kike sita na kiume watano.
Na kati ya watoto hao wa kiume, mmoja ana siku tano tangu kuzaliwa kwake, na amepewa jina la Hillary ambaye ni baba yake mkubwa.