Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob Mkunda leo amewaaga rasmi maofisa sita wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambao wamestaafu baada ya kulitumikia jeshi kwa zaidi ya miongo mitatu.

Maofisa hao wa jeshi ni Mameja Jenerali, Gabriel Mhidze, Charles Mbuge, Ally Katunde na Chelestino Msolla wakati Mabrigedia Jenerali ni William Likangaga na Andrew Mugamba.

Jenerali Mkunda amesema kuwa ni furaha kubwa kuwaaga majenerali hao kwa aina hiyo ya hafla, yaani kwa kuwasukuma katika magari ya wazi hadi nje ya geti la katuka Kambi ya Twalipo, Mgulani Dar es Salaam.

Amesema hao majenerali wataendelea kuwa sehemu ya jeshi hilo na wakati wowote watakapowahitaji watawatumia hadi baada ya miaka mitatu.