Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wabunge wanaoshiriki mashindano ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wayatumie kuimarisha ushirikiano.
Ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Desemba 4, 2017) wakati akifungua mechi ya mpira wa miguu iliyozikutanisha timu za Tanzania na Burundi kwenye Uwanja wa Taifa.
Mashindano hayo ya Nane ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yalifunguliwa jana (Jumapili, Desemba 3, 2017) na Spika wa Bunge Job Ndugai
Waziri Mkuu amesema nchi zote zinashiriki mashindano hayo ni ndugu hivyo ni vema wakayatumia katika kuimarisha ushirikiano wa Mabunge ya Jumuiya hiyo.
Pia Waziri Mkuu amewataka wachezaji hao kuhakikisha kucheza mpira mzuri na wazingatie viwango vya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).
Hata hivyo Waziri Mkuu amesema katika mashindano hayo kila timu inahitaji kupata ushindi, hivyo amewataka wanatumie vizuri ujuzi wao ili waibuke na ushindi.
Katika ufunguzi huo Waziri Mkuu aliambatana na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Akson, Katibu wa Bunge la Tanzania Stephen Kagaigai.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe.
Katika mashindano hayo timu ya Tanzania imeibuka kidedea baada ya kushinda magoli matatu na Burundi ilipata magoli mawili.