Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kisongo Arusha ambako alifungua Maadhimisho ya Wiki ya Huduma ya Fedha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini humo, Novemba 22, 2023. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela na wa tatu kushoto ni Waziri wa Fedha, Dkt Mwigulu Nchemba.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anjela Mziray (kushoto) wakati alipotembelea banda la maonesho la mfuko huo kabla ya kufungua Maadhimisho ya Wiki ya Huduma ya Fedha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha , Novemba 22, 2023. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajasiriamali wakati alipotembelea banda la maonesho la Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kabla ya kufungua Maadhimisho ya Wiki ya Huduma ya Fedha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Novemba 22, 2023. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Profesa, Joyce Ndalichako (kulia ), Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Theobald Sabi takati alipotembelea banda la maonesho la NBC kabla ya kufungua Maadhimisho ya Wiki ya Huduma ya Fedha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Novemba 22, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)