Majaliwa amwakilisha Rais Samia ibada ya mazishi ya Membe Rondo
JamhuriComments Off on Majaliwa amwakilisha Rais Samia ibada ya mazishi ya Membe Rondo
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 16, 2023 amemuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ibada ya mazishi ya Marehemu Bernard Membe iliyofanyika kijijini kwake Rondo, Chiponda Mkoani Lindi.
Akizungumza na waombolezaji katika ibada hiyo Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania kumuombea na kuenzi yote mazuri aliyowahi kufanya marehemu Bernard Kamilius Membe wakati wa uhai wake.