Na Tatu Saad, JAMHURI MEDIA
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Imemwachilia huru Amani Philipo Mkazi wa Mbezi Dar es Salaam aliyefunguliwa mashitaka ya mauaji kwa kukusudia ya sajent Mensah wa kituo Cha polisi mabatini,kijitonyama.
Uamuzi huo umetolewa Leo Machi 20, mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Romuli mbuya, baada ya kutokumkuta na hatua ya mauaji ya askari huyo.
Mbuya ameeleza kuwa, upande wa mashitaka ushahidi wake ulikuwa na mapengo mengi hivyo umeshindwa kithibitisha kuwa mtuhumiwa alikuwa amehusika na kifo Cha sajent mensah.
Katika kesi hiyo ilidaiwa Amani Philipo mnamo Julai 22,2016 usiku alimuua Sajenti Mensah maeneo ya mataa ya sayansi Dar es Saalam Kwa kumpigia risasi ya kifua upande wa kulia.
Mbuya aliieleza kuwa risasi hiyo ilisababisha kuvunjika Kwa mbavu na kutobolewa Kwa mapafu ambapo jeraha hilo lilisababisha kuvuja Kwa damu nyingi na kupelekea kifo Cha marehemu.
Mbuya alidai marehemu sajent Mensah akiwa na mwenzie Inspecta Ashiraf wakiwa katika kituo Cha kuongozea magari kilichopo njiapanda ya sayansi walivamiwa na kupigwa risasi ambapo mshitakiwa alihusishwa Kwa kutambuliwa na shahidi namba Moja ambaye ni Ashiraf.
Akisoma hukumu hiyo mbuya amedai, upande wa mashtaka walileta mashahidi sita na vielezo sita ambapo katika vielezo hivyo kulikuwa na taarifa ya uchunguzi wa kifo,ramani ya tukio, maelezo ya shahidi namba 1, maelezo ya shahidi namba 3, maelezo ya shahidi namba 4 na onyo la polisi na Kwa upande wa utetezi mshitakiwa alieleza mwenyewe na shahidi mmoja ambaye siku hiyo ya tukio walishinda wote.
Mbuya ameeleza kifo cha sajent Mensah kilithibitisjwa mahakamani hapo na shahidi namba 2, alipokabidhi kielelezo cha uchunguzi wa mwili ambapo aliieleza kuwa mwili wa marehemu ulikuwa na jeraha la risasi lenye urefu wa sentimita 3, kuvunjika Kwa mbavu na mapafu yalitobolewa.
Pia alidai kuwa ushahidi wa Inspecta Ashiraf ulikua ni ushahidi wa utambuzi bila kielelezo kilichoonesha muonekano wa mtuhumiwa.
Hakimu Mbuya ameeleza kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka, mtuhumiwa amehusishwa na mauaji hayo Kwa kutambuliwa eneo la tukio na utambuzi uliofanyika kituo cha polisi ostabey na hakuna shahidi aliepeleka kielelezo kilichoonyesha muonekano wa mtuhumiwa na jinsi gani aliweza kumtambua.
Amefafanua kuwa mamlaka mbalimbali zimeonyesha ushahidi wa utambuzi ni ushahidi dhaifu na usio aminika na ushahidi huo umezikanya mahakama kutumia katika hukumu isipokuwa ushahidi huo utakapokuwa ni mzito sana.
Pia amedai Kwa kuzingatiaa aina hii ya ushahidi unapaswa kuzingatia mambo matatu ambayo muda ambao mtambuzi alichukua kumtambua,mazingira ya utambuzi,kama mtambuzi alikuwa anamfahamu mtuhumiwa.
Mbuya ameeleza kuwa shahidi Ashiraf alidai kuwa wavamizi hao waliwavamia kutoka nyumba ya Banda na alipojaribu kugeuka ili atazame kinachoendelea alisikia mlio wa risasi ndipo alipotafuta namna ya kujiokoa, Kwa vyovyote alikuwa na hali ya kuogopa na alisema matukio hayo yalifanyika Kwa dakika Moja ambapo muda huo shahidi alikuwa makini kwenye kuokoa maisha yake na sio utambuzi.
Hakimu Mbuya pia ameeleza katika ushahidi wa Askari uliotolewa na upande wa Jamhuri ulieleza kuwa Mtuhumiwa alikamatwa nyumbani kwake baada ya polisi kupewa taarifa na msili wao na hawakueleza kama mshitakiwa alikamatwa kulingana na vigezo alivyovieleza mtambuzi.