Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Ian Wright anasema kuwa hakuna sababu za kusalia kuwa meneja baada ya msimu huu.
Wright pia aliwashutumu baadhi ya wachezaji kwa kutojituma na kudai kwamba mmiliki wa klabu hiyo Stan Kroenke hajali.
Arsenal imepoteza mechi sita kati ya 12 2018, ya hivi karibuni ikiwa fainali ya kombe la Carabao dhidi ya Manchester City.
‘Wenger amekuwa akitoa sababu na kwamba anawapendekeza na kuwatetea wachezaji wake’, Wright aliambia bbc radio 5 live.
‘ Iwapo atasalia msimu ujao sioni sababu na sidhani kwamba mtu yeyote anaweza kufanya hivyo. mambo kama haya ni sharti yafikie ukingoni’.
Akizungumza siku ya Jumatatu , Wright ambaye alifunga magoli 158 kati ya mechi 288 alizoichezea Arsenal na kustaafu katika kandanda 2000 alizungumzia kuhusu haya:
- Malengo kwa Arsenal kusonga mbele.
- Mmiliki wa Arsenal anafaa kuchukua udhibiti
- Viwango vinavyohitajika kwa Mkufunzi mpya wa Arsenal.
- Iwapo Henry anapaswa kumrithi Wenger.
‘Ni Safari ndefu’
Arsenal imeshinda mataji saba ya FA chini ya Wenger ikiwelo lile la msimu uliopita lakini mataji matatu ya mwisho ya EPL yalipatikana chini ya raia huyo wa Ufaransa mwaka 2004.
Wright: “nataka Arsenal ipiganie mataji tena , waweze kusajiliwachezaji ambao wanaweza kukufurahoisha nataka mkufunzi ambaye atawaongoza .Baadhi ya wachezaji hawajitumi kwa sababu wanamiliki mali ambazo wanakodisha. Ni muda gani ambao Arsenal itachukua kurudia ufanisi wao. Kila timu inafanikiwa na kusonga mbele katika zile timu tano bora .Arsenal inarudi chini lazima wasitishe mwelekeo huo , watafute mkufunzi mzuri na baadaye kutafuta wachezaji watakaosonga mbele. Safari ndefu.
‘Mwenyewe lazima ashirikishwe‘
Raia wa Marekani Stan Kroenke amekuwa mwenye hisa mkubwa wa Arsenal tangu 2011 akiwa na asilimia 66.6 huku bilionea raia wa Urusi Alisher Usmanov akishikilia asilimia 29.9.
Wright: Mimiliki wa Arsenal ni sharti abebe lawama kwa tatizo hili. Kroenke hajali , na iwapo anajali Wenger asingepewa kandarasi mpya ya miaka miwili.
”Kila mtu anaweza kuona kwamba imefikia mahali ambapo Wenger anahitaji kuondoka”.
”Mwenyewe lazima ashirikishwe ili ajue kinachoendelea , ni vipi, na ni nini tutafanya, ni vipi tutarudi katika kiwango tulichokua zamani. Mashabiki wamekuwa wakisema kwa miaka kadhaa lakini hakuna mtu anayesikiliza”.
”Mimiliki hajasema chochote na amemwachia Wenger kuendelea. hakuna kuwajibika kwa wachezaji . hakuna kufuatilia msururu wa matokeo mabaya kwa hivyo wanaendelea wanachopfanya”.
‘Arsenal wanahitaji mtu mwenye mwelekeo‘.
Mkufunzi wa zamani wa Chelsea Carlo Ancelotti amehusishwa na hatua ya kumrithi Wenger pamoja na kocha wa Napoli Maurizio Sarri. Wenger ameiongoza timu hiyo tangu 1996.
Wright: “Arsenal inafaa kuanza kumsaka kocha ambaye sio mzee. Wanazungumzia kuhusu Ancelotti lakini wanafaa kutafuta mtu kama Mauricio Pochetinno ambaye alijijenga.
”Marco Silva ni kocha mwengine ambaye ameonyesha uwezo wake .Mtu kama yeye anaweza kuijenga timu na kuwa na falsafa yenye malengo, mtu anayeweza kuleta mchezaji ambaye atafanikisha falsafa yake kama tunavyoona katika klabu ya Manchester City”.
‘Hatujui kile Henry anachoweza kufanya‘
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Thierry Henry, akiwa miongoni mwa makocha wa timu ya Ubelgiji alipendekeza wakati alipokuwa akiifanyia kazi Sky Sports siku ya Jumapili kwamba huenda akaifunza klabu hiyo katika siku za usoni. Alipoulizwa kuhusu kazi hiyo Henry alisema: Hana hamu.
Wright: “Thierry ni mfalme hapa. Lakini kwa yeye kuja hapa akiwa naibu mkufunzi kutoka Ubelgiji na kuchukua ukufunzi wa Arsenal wakati wa mazingira yaliopo sasa na mabadiliko yanayohitajika tutazungumza kuhusu mchezaji maarufu ambaye ataubeba ulimwengu wa Arsenal wakati ambapo mambo hayaendi vyema katika mabega yake.
”Arsenal haipo katika wakati ambapo inaweza kumfuta Wenger ambaye tunampenda sana lakini ambaye unapomtaja miongoni mwa mashabiki wengine wanakunja uso.Watu wamekasirika”.
”Nisingependelea hilo kufanyika kwa Henry kwa sababu amechukua kazi hiyo mara tu baada ya Wenger kuondoka. Itakuwa vigumu amefunza kwa hivyo hatujui ni nini anachoweza kufanya .
Ni wazo ambalo linahitaji kufikiriwa kwa undani na kufanyiwa kazi.Sidhani kwamba tunaweza kuendelea na hali ilivyo sasa”.