Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Morogoro
Magwiji 27, wakiwemo wacheza gofu ya ridhaa na kulipwa wamefuzu mchujo wa kucheza raundi ya tatu ya michuano maalum ya gofu kumuenzi mama Lina Nkya baada ya kufanya vizuri katika raundi mbili za awali katika viwanja vya gofu vya Morogoro, mjini Morogoro jana na juzi.
Orodha ya wachezaji hao magwiji inaongozwa na mchezaji wa ridhaa, Ally Isanzu kutoka klabu ya TPC ya Kilimanjaro ambaye hadi jana alikuwa amepoteza fimbo 147 na kuwashinda wapinzani wake wakubwa kwa fimbo moja.
Kewa mujibu wa Mkurugenzi wa mashindano hayo Hassan Nkya amesema katika orodha ya waliofanikiwa kupita mchujo, kuna wachezaji 13 wa kulipwa na 14 wa ridhaa.
Isanzu, ambaye aliyaanza mashindano hayo kwa kupiga mikwaju 74, jana aliboresha uchezaji wake kwa kupiga fimbo 73 ambayo ni juu ya kiwango kwa fimbo moja.
Nafasi ya pili inashikiliwa Hassan Kadio aliyepiga mikwaju 148 baada ya jana kupata mikwaju 75.
Bryson Nyenza, ambaye aliongoza siku ya kwanza jana alimaliza katika nafasi ya tatu kwa kupiga jumla ya mikwaju 150. Nyenza ameungana na Nuru Mollel wa Arusha ambaye pia amepoteza fimbo 150 katika siku mbili za michuano hiyo.
Isihaka Daudi wa TPDF Lugalo anajiunga na Mollel katika nafasi ya tatu kwa alama hiyo hiyo.
Aidha orodha ya wachezaji waliofuzu mchujo pia inawajumuisha Abdallah Yusuph, Seif Mcharo John Said na Isaack Wanyeche. Wengine ni Victor Joseph,Vicky Elias, Karim Ismail ambao wanaungana na mchezaji wa kulipwa, Salum Dilunga Ninja.
Pia wapo katika orodha ya waliofuzu ni Geoffrey Leverian, Fadhil Nkya, Frank Mwinuka, Athuman Chiundu, Michael Massawe,George Sembi,Enoch Wanyeche,Madina Iddy na Baraka Samuel.
Wengine ni Godfrey Gwacha,Ibrahim Mtemi,Neema Olomi na Angel Eaton.
Mashindano ya Lina Golf Tour ni mfululizo wa michuano ya gofu kwa ajili ya kumuenzi mlezi wa gofu ya wanawake Lina Said Nkya ambaye alifanya kazi kubwa ya kuikuza gofu ya wanawake nchini.