Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar ea Salaam
Mageuzi makubwa yaliyofanyika kwenye sekta ya Afya nchini kupitia Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan yameivutia Serikali ya Jimbo la Kilifi kutoka Kenya ambao wamefika kujifunza namna Tanzania ilivyofikia hatua hiyo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya
Jimbo hilo Peter Samwel Mwarogo akiwa na Wabunge wa Kamati ya Afya ya Jimbo hilo ambao wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili kuona mageuzi kupitia huduma, uwekezaji vifaa tiba, uboreshaji miundombinu na utawala.
“Tumekua tukisikia maboresho ya huduma Tanzania hususani Hospitali ya Taifa Muhimbili hivyo tumekuja kujifunza mambo mengi mtambuka ili tukaboreshe sekta ya Afya kwa ujumla wake katika Jimbo letu” amesisitiza Mhe. Mwarogo.
Ameongeza kuwa ni muhimu kujifunza kutoka Tanzania kupitia *Muundo wa Kusini Kusini” ambapo mazingira yao na Tanzania yanafanana hivyo kurahisisha utekelezaji wa yote waliyojifunza.
Kwa upande wake Mwenyekiti kamati ya Bunge ya Afya wa Jimbo hilo Edward Zero, amesema wameona mambo mengi ambayo ni chachu kwao kwenda kuyafanyia kazi.
Pamoja na hayo wamejadiliana na Menejimenti ya Hospitali kuhusu usimamizi wa Hospitali, kusomesha watalaam, ununuzi wa dawa na vifaa tiba, malipo ya huduma kwa makundi mbalimbali.
Aidha, wameelezwa kuhusu uendeshaji wa mtambo wa kuchoma taka, uendeshaji Kliniki za wagonjwa wa kulipia, uwajibikaji wa watumishi, uendeshaji Idara ya dharura, radiolojia na masuala mengine mengi