Serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO imetoa onyo kwa magazeti matatu nchini kutokana na kile ilichoeleza kuwa ni kukiukwa kwa maadili ya uandishi wa habari.

Hayo yalisemwa jana na Dkt Hassan Abbas ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali ambapo alisema miongoni mwa magazeti hayo ni pamoja na gazeti la Tanzanite. Magazeti hayo yalipewa onyo katika kipindi cha mwezi Februari na mwezi Machi mwanzoni.

Akitaja sababu za gazeti la Tanzanite kuonywa, Dkt Abbas alisema ni kutokana na kukiuka maadili kwa kuchapisha picha za nusu utupu za mwanadada Mange Kimambi.

“Moja ya magazeti yaliyooonywa na pamoja na gazeti la Tanzanite, tumewaonya kwa sababu ni mara yao ya kwanza kuchapisha picha fulani za utupu sio kuhusu content (habari), ni kuhusu aina ya picha walizochapisha,”alisema Dkt Abbas.

Amesema kuwa hatu hizo zimekuwa zikichukuliwa kwa magazeti mbalimbali kwa nia njema ya kuhakikisha kunakuwapo na weledi katika utendaji kazi ya uandishi wa habari.

Aidha, amesema wameendelea kuchua hatua kwa upande wa runinga ztakazokiuka maadii ya uandishi.