Maafisa nchini Cameroon wamesema mafuriko ya karibuni yamesababisha watu 70,000 kutoka katika kambi za muda ambazo zilianzishwa na watu walioathiriwa na mafuriko kwenye mpaka wa kaskazini wa nchi hiyo na Chad na Nigeria.
Baadhi ya watu walioathirika na mafuriko sasa wamehamia katika nchi jirani ya Chad, ambako takriban watu milioni mbili wamekuwa wakiishi katika kambi maalum za mafuriko.