*Waorodhesha simu, majina hewa ya watu
*Mbinu hiyo yawafanya watumbue
mamilioni
*Watumishi 11 wakiona cha moto,
wafukuzwa
ARUSHA
NA MWANDISHI WETU
Ufisadi wa mamilioni ya shilingi umebainika
kufanywa kwenye miradi ya baiogesi
inayosimamiwa na Kituo cha Zana za Kilimo
na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) mkoani
Kilimanjaro.
CAMARTEC ilianzishwa kwa Sheria Na. 19
ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Novemba, 1981.
Lengo lake ni kuinua hali ya maisha ya
wananchi vijijini kupitia maendeleo, maji,
ujenzi wa nyumba za gharama nafuu,
usafiri, nishati mbadala na ushughulikiaji wa
mazao baada ya kuvunwa.
Majina na mitambo ‘hewa’ vimebainika
kuwapo kwenye mradi huo, kiasi cha
kufanya CAMARTEC ipoteze Sh bilioni 1.2.
Kiasi kikubwa cha fedha hizo kimetoka kwa
wafadhili ambao ni nchi ya Uholanzi.
JAMHURI limechapisha orodha ya majina
ya watu na maeneo ambako ‘mitambo
hewa’ ya baiogesi inadaiwa kujengwa.
(Tazama vilelezo).
Ufisadi huo umejulikana kupitia taarifa ya
uhakiki (physical verification) ya Aprili,
mwaka jana iliyoonyesha kuwapo ‘mitambo
hewa’
,
‘majina hewa’ ya wanufaika na
majina ya kughushi ya wananchi
wanaodaiwa kunufaishwa na mitambo hiyo.
Baiogesi ni nishati jadidifu inayotokana na
kinyesi.
JAMHURI limeelezwa kuwa miongoni mwa
mitambo ya baiogesi 4,475; mitambo 860
miongoni mwa hiyo haifanyi kazi.
Pamoja na kuwapo ufisadi huo, JAMHURI
limethibitishiwa kuwa malipo kwa wahusika
wa ‘mchezo’ huo yamekwisha kufanywa.
Majina ya ‘wananchi hewa’ yameingizwa
kwenye orodha ya wale
wanaodaiwa kunufaishwa na huduma hiyo,
jambo ambalo wakaguzi wamebaini kuwa si
kweli.
Baadhi ya majina yaliyoandikwa kwenye
ripoti ya mradi, wenye majina hayo ama
hawapo au hawajulikani hata kwa wanavijiji.
Wengine wamewekewa namba za simu
kuonyesha kuwa ni za wanufaika wa mradi
huo, lakini uchunguzi umebaini kuwa baadhi
ya namba hizo hazina wateja na nyingine
zinamilikiwa na watu tofauti walio nje ya vijiji
vinavyotajwa.
Idadi kubwa ya majina kwenye orodha ya
CAMARTEC wanadaiwa kujengewa
mitambo ya baiogesi, lakini uchunguzi
uliofanywa kwa kwenda katika maeneo
husika umebaini kuwa watu hao hawapo.
Kwenye mlolongo huo, asilimia 92 ya
mitambo hiyo katika Mkoa wa Kilimanjaro
ambayo inasemekana ipo, haikujengwa
(mitambo hewa).
Chanzo cha habari kimelieleza JAMHURI
kwa kutoa mfano kuwa mitambo ya baiogesi
ambayo ripoti inaonyesha inamilikiwa na
Evans Njau mwenye namba ya simu
0767373449 na Laurent Benedict
(0713318556) wa vijiji vya Useli na Kanji
mkoani Kilimanjaro; haipo.
Namba hizo za simu ni za Benedict
Laurance Samky anayeishi Dar es Salaam;
na hana mtambo wowote aliojengewa
kwenye makazi yake.
Patrick Samson (0757755090) anayeishi
Kinyamvuo, anaonyeshwa kuwa alijengewa
mtambo mwaka 2016; lakini yeye
mwenyewe amekanusha. Badala yake,
mtambo uliopo ulijengwa mwaka 2013
kama mtambo wa majaribio na Kampuni ya
Mwika Biogas wakishirikiana na Patrick
Samson.
Kwenye ufisadi huo, asilimia 10 ya mitambo
11,103 (takriban mitambo 1,110)
imeripotiwa zaidi ya mara moja kuwa ipo.
Mitambo mingine haina nyaraka za
kuthibitisha kama kweli ipo.
“Mtambo huo huo mmoja unaripotiwa kuwa
upo kijiji fulani, halafu unaonyeshwa uko
kijiji kingine, kisha unaonyeshwa uko kijiji
kingine tena,
” kimesema chanzo chetu.
Kwenye mlolongo huo, ufuatiliaji uliofanywa
umebaini mambo mengine kadhaa. Mosi,
familia 6,441 miongoni mwa familia 9,570
ambazo ni sawa na asilimia 67.3 ni ‘familia
hewa’
, yaani hazipo, lakini zinaonekana
kwenye mafanikio ya CAMATERC ya watu
waliopata huduma za mradi wa baiogesi.
Pili, familia 3,129 miongoni mwa familia
9,570 ya familia zilizopatikana; miongoni
mwake, familia 1,095 zimesingiziwa kuwa
zinamiliki mitambo ya baiogesi wakati
ukweli ni kwamba hazina kabisa huduma
hiyo.
Tatu, familia 2,034 zimebainika kuwa ni zile
ambazo zilikuwa na mitambo ya baiogesi
isiyofanya kazi, lakini kwenye ripoti
inaonyesha kuwa iko barabara.
Utafiti huo ni mwendelezo baada ya ule wa
awali uliotoa mwanga wa kuwapo ufisadi.
Utafiti huo ulifanywa na Kampuni ya Gold
Standard mwaka 2016. Kwenye utafiti wao,
ilibainika kuwa familia 65 miongoni mwa
familia 120 zilikuwa zimesingizwa
kujengewa mitambo ya baiogesi.
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa
CAMATERC, Profesa Siza Tumbo, ambaye
kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Kilimo na Chakula, amezungumza na
JAMHURI na kukiri kuwapo kwa ufisadi huo.
Amesema amedumu kwenye taasisi hiyo
kwa miaka miwili, na kwamba yote
yanayosemwa aliyakuta, akajitahidi
kuyatafutia suluhu na anaamini uongozi
uliofuata baada yake utalikabili tatizo hilo.
“Nilianza kazi rasmi Aprili 11, 2016, haya
yote yametokea nikiwa sipo. Mengi, yote
yakiwamo ya baiogesi nimelikuta.
Mkurugenzi Mkuu aliyekuwapo (Elfariji
Makongoro) alifariki dunia Desemba 2015.
Kama angekuwepo labda ndiye angeweza
kujibu,
” amesema Profesa Tumbo na
kuongeza: “Matendo haya maovu
nimeyakuta, sijashiriki kwenye hatua
yoyote.”
Amesema hadi anaondoka CAMARTEC,
ufisadi kwenye mradi wa baiogesi ulikuwa
ukichunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru).
“Mimi ndiye niliyepeleka suala hili Takukuru.
Mradi huu ulikuwa mkubwa. Ulianza mwaka
2009 ‘phase one’ (2009-2013), baadaye
awamu ya pili ilikuwa mwaka 2014-2017.
Kitu kikiwa kwenye uchunguzi si vizuri
kukizungumza. Mimi nilianza kazi Aprili
2016, ilipofika Juni wafadhili wakaomba
tuonane. Walipokuja wakaongelea ‘mitambo
hewa’ – wakasema mingi sana iko Moshi.
“Nikaita nyaraka zote za internal auditor
(mkaguzi wa ndani), sikukuta sehemu
yoyote ya maana ikizungumzia mitambo
hewa. Nikasafiri kwenda huko kwenye
mitambo, nikafika Bomang’ombe, Sanya
Juu. Ndani ya saa mbili nikathibitisha
kuwapo ‘mitambo hewa’. Nikarudi kwenye
taarifa ya ofisini sikuona kama hili suala
limeandikiwa taarifa. Nikamwita mhusika
(mkaguzi) nikamuuliza vipi tatizo kubwa
kama hili halijulikani?
“Akaniambia kuwa co-ordinator (mratibu)
anamzuia, nikaona rubbish. Baada ya
kumbana ndipo akaandika taarifa. Lakini
wakati huo wafadhili walishafanya ukaguzi
mara mbili au tatu.
“Tukakaa na wafadhili kufuatilia mitambo
hewa yote A-Z. Mwaka 2017 tukafanya kazi
hiyo kuanzia Machi – Juni, 2017. Kazi
ilikuwa ngumu, maana mitambo 13,000 nchi
nzima si mchezo. Tukatuma timu kuainisha
mitambo kwa kutumia GPS.
“Nikazungumza na wafadhili ili wao
wenyewe waone mkaguzi anayefaa.
Wakaleta wakaguzi PWC kutoka Kenya.
Matokeo ya uchunguzi yakasaidia bodi
kuwaondoa wafanyakazi 11 wote wa mradi
mwaka jana,
” amesema Profesa Tumbo.
Uchunguzi ulibaini kuwa wafadhili nao
walikuwa washiriki wa ufisadi huo.
“Walikuwa sehemu ya udhaifu. Mimi
nimekuta matukio yapo, nimeyapeleka
Takukuru. Wafadhili walikubali kuendelea
na ufadhili baada ya sisi kuonyesha
ushirikiano wa hali ya juu,
” amesema
Profesa Tumbo.