Wiki iliyopita katika kitabu hiki cha Maendeleo ni kazi mwalimu alikuwa anazungumzia kuhusiana na sera ya Kuanzisha vijiji vya ujamaa na namna ya kuzingatia vipaumbele vya msingi katika kuwaletea maendeleo wananchi. Sehemu inayofuata ni mwendelezo wa pale tulipo ishia wiki iliyopita.
Kwamba mahala pa kujenga maskani nyumbani, shule, viwanda, hospitali ni pale; kwa hiyo Mheshimiwa kajenga pale siyo hapa. Hapa tunakusaidia kupanda vitu. Hili si jambo la ajabu hata kidogo. Dar es Salaam hatauachi tu ukajijengea mahala popote tu hapa, hata mahala tulipokusudia kupitisha barabara wewe unakuja kujenga tu. Tukikuambia kwanini unajenga hapa unaniambia mwongozo wa Ibara ya 15. Ibara ya 15 imekuambia ujenge mahala popote tu? ( vicheko.)
Kwa hiyo nasema katika Halmashauri Kuu tulikubaliana nchi nzima sehemu zote, najua sehemu zenye matatizo; lakini siyo sehemu zote zenye matatizo. Twende tufanye mipango ya kuishi vijijini. Na sehemu nyingine tumekwenda, sehemu zimekwisha pimwa, maeneo yamekatw, maeneo ya vijiji yale yamekwisha katwa na sehemu za kuishi zimepimwa zimekwisha, kilichobaki ni kutekeleza. Sasa viongozi wa TANU; kwa mfano nimetoks Mkoa mmoja nimeambiwa wamekaa wameita mkutano wa Mkoa wa mwaka ule, mkutano wa mwaka umekaa umezungumza jambo hili umekubaliana haya tayari tuhame sasa, mwaka huu tutahamia katika maeneo gani, yametamkwa maeneo yale mara yamekwisha pimwa sasa wamedhani jambo zuri sana, katika mkutano huo wa mwaka. Wamesema wa kwanza kuhama wawe viongozi (makofi) unaona makofi madogo sana hapo (makofi na vicheko).
Sasa Waheshimiwa hili itakalosema bay asana hili. Hili nitakalo sema sasa hivi bay asana. Wamesema katika mkutano huo kwamba wa kwanza kabisa viongozi na hili kweli safi kabisa. Dodoma ndivyo walivyofanya. Waliita mkutano wa viongozi baada ya mwaka mzima kabisa walielezana yamekwisha waliita mkutano wa viongozi, wakapiga semina ya viongozi wakapitisha azimio lao viongozi wenyewe wahamie katika vijiji; na wakahama viongozi wakahama katika vijiji maeneo yamekwisha pimwa wakahamia katika vijiji. Nakumbuka Dododma nimekwenda sehemu moja nimeshangaa san asana. Mheshimiwa mmoja Chifu wa zamani eneo lake lile lile. Lakini yuko upande mmoja yako kule ni pale pale katika eneo la kijiji. Sasa wanaambiana wahame na viongozi wawe wa kwanza kuhama na kuhama ni kuvunja tembe uvunje tembe uondoke uende mahala hapo. Huyu chifu wa zamani amevunja; bure, amevunja kwa sababu anasema kama sikuvunja wengine watu wangu siyo kwamba wako tu hawa watu ambao ninawaongoza, wengine wako huko wnatazamiwa waje hapa: sasa wataniona mimi nimekaa tu. Basi madhali wao wanahangaika kuvunja matembe yao huko waje hapa, nami ninavunja langu. Navunja la kwangu halafu nitasogea nitajenga pale. Basi kavunja makusudi kabisa halafu akasogea akajenga pale. Kiongozi huyo, (makofi). Kiongozi huyo- Chifu wa zamani. Hajui hotuba hajui chochote, anajua kuongoza tu. (Kicheko).
Sasa wamefanya na wala msione ajabu kwamba eh! Wala msionre ajabu baada ya hapo ilikuwa watu lazima watakwenda mathali viongozi wamekwisha fanya hivyo ni kuwaq watu lazima watahama; na wamehama. Dodoma hivi sasa imebaki sehemu ndogo sana ya watu ambao hawajahamia vijijini. Sasa katika mkoa huo ninaousema nimekwenda nimekuta wamepitisha azimio hilo. Sasa viongozi bado wanasema ah, sasa lazima tuanze sisi kwa nini? Kwa sababu wnanchi wanasema. Ikiwa jambo hili ni jema hili jaqmbo mnalotueleza kama ni jema anzeni nyie ( makofi).
Sasa jema katika jukwaa tu. Kama ni jema anze3ni nyie. Sasa wah3eshimiwa nalirudia hilo kwamba haya tunayose3ma ya utekelezaqji haya tumesema msingi wake mmoja ni kukaa pamoja. Hivi tutajisemea tu samaki ziko wapi, maji yako wapi?. Msingi wa kukaa pamoja ni jambo zito, na zuri na matumaini yangu ni kwamba tutalitekeleza na mimi mwakani naahidi hivyo maana kazi yangu moja mathali maana ni siasa ya chama, kukaa pamoja ni siasa ya chama ni siasa yenu mmwkwisha isema wenyewe, Halmashauri kuu imesema sasa tusiseme tena Mkoa mmoja mmoja tuseme nchi nzima. Sasa kazi yangu mimi na wenzangu ni utekelezaji. Nimepita huko nimewaambia wenzangu kwamba tutatekeleza, kilichobaki ni utekelezaji ni siasa ya chama mwongozo wa Halmashauri Kuu tumekwisha pata kilichobaki ni kutekeleza. Kazi yetu ni kutoa taarifa ya utekelezaji.
Sasa mwakani kuna mkutano wa uchaguzi waheshimiwa na tutachagua viongozindiyo sasa sitaki kulisema tena zaidi (makofi).
Tangu tumekutana ndiyo tumefanya jambo la madaraka mikoani mnajua waheshimiwa mtatueleza tutakapofika huko mbele ya safari tumeendelea kiasi gani.
Habari ya Elimu ya Msingi- elimu ya msingi tumepiga hatua kidogo. Kwa mjibu wa hesabu nilizopewa mwaka 1971 tulikuwa na watoto laki tisa na mbili elfu na mia sita, waliokuwa katika shule za msingi. Mwaka huu nimeambiwa, niliambiwa mapema nadhani idadi hii ilichukuliwa kabala ya kuanza kuwachukua wapya wakati waliokuwamo mwanzoni tulikuwa na watoto wa shule katika shule za msingi tulikuwa na watoto milioni moja na laki moja sitini na mbili elfu na mia tano katika shule.
Lakini ingawa hesabu hiyo imeongezeka hivyo nitawarudisheni nyuma ingawa hesabu imeongezeka kama kama idadi ya watoto milioni moja na laki moja sitini na mbili elfu na mia tano katika shule. Lakini ingawa hesabu hiyo imeongezeka kama idadi ya watoto wetu ingekuwa ni ile ile kila wakiongezeka maana yake ndiyo kusema wasiosoma wanapunguka. Lakini usije ukadanganywa na kuongezeka kwa watoto madarasani ukadhani una punguza wasio soma.
Si kweli hata kidogo. Kwa sababu wakati ule ule wanaongezeka; kwa hiyo naambiwa kwamba idadi ya kweli ya kweli ya watoto wanaoweza kuingia katika darasa la kwanza katika shule zetu za msingi hata leo hivi yaani mwaka huu ni 48.6 kwa mia tu ya watoto wenye umri wa miaka saba katika nchi yetu.
Ndiyo. Kwa hiyo usije ukadanganywa na hesabu hiyo na mimi sipendi kudanganywa danganywa- usije ukadanganywa na hesabu hiyo kwamba mwaka 1971 tulikuwa na watoto laki tisa sasa tuna watoto milioni moja na laki mbili ukadhani kwa hiyo tumepiga hatua kubwa. Ndiyo tumepiga hatua kubwa. Lakini bado watoto wengi hawasomi. Na mpaka idadi hiyo imeongezeka kiasi cha 1 kwa mia tu kwa mwaka. Ndiyo kusema kwamba tusipo harakisha mpango wetu wa kupanua elimu ya msingi hatutaweza kumsomesha kila mtoto anayefikia umri wa miaka saba mpaka mwaka wa 2034.