Dunia inaendelea kuomboleza kifo cha kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis, aliyeaga dunia Jumatatu wiki hii akiwa na umri wa miaka 88, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Dunia inaendelea kuomboleza kifo cha kiongozi wa Kanisa Katoliki dunianiPapa Francis, aliyeaga dunia Jumatatu wiki hii akiwa na umri wa miaka 88, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Makumi ya maelfu ya watu wanatarajiwa kuendelea kujitokeza hii leo kuuaga mwili wa kiongozi huyo kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Asubuhi ya leo zoezi hilo litafunguliwa kuanzia majira ya saa moja asubuhi hadi saa moja jioni kwa saa za Vatican.

Duru za ndani kutoka Vatican zinakadiria kwamba kufikia jana jioni watu 20,000 walikuwa tayari wameshautazama mwili wa papa huku karibu watu 100,000 walikuwa wamekusanyika nje kwenye Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro wakisubiri nafasi hiyo.

Maziko ya Papa Francis yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi.