Diwani wa Kata ya Ukenyenge, Anderson Mandia, Wilaya ya Kishapu akizungumza katika mkutano wa madiwani wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao.

Afisa Programu, Uchechemuzi wa TGNP Mtandao, Deogratius Temba (kulia) akiwasilisha mada katika mkutano wa madiwani wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao.

Diwani wa Vitimaalum-Mwadui, Sarah Masinga (kulia) akizungumza katika mkutano wa madiwani wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao.

Diwani wa Kata ya Nsalala, Kissman Mwangomale akizungumza katika mkutano wa madiwani wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao.

BAADHI ya madiwani walioshiriki katika mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao, wameipongeza TGNP Mtandao na kuiomba kupanua shughuli zake mikoa mbalimbali ili kuchochea shughuli za maendeleo hasa ya miradi anuai.

Mkutano huo ulioshirikisha madiwani zaidi ya 20 kutoka Halmashauri ya Wilaya za Kishapu, Tarime, Mbeya, Morogoro Vijijini na Manispaa za Ilala, Kinondoni na Ubungo za jijini Dar es Salaam, wakichangia mjadala waliitaka TGNP kupitia programu yao ya vituo vya taarifa na maarifa kuenezwa mikoa mingine kwani vinachochea shughuli za maendeleo.

Diwani wa Ijombe, Stimar John akizungumza katika mkutano huo aliishauri TGNP Mtandao kuongeza maeneo ya kufanyia kazi kupitia mradi wao wa vituo vya taarifa na maarifa kwani baadhi ya maeneo vimekuwa chachu ya maendeleo kuhimiza sehemu ya miradi ya maendeleo.

“…Awali wakati TGNP Mtandao ikiingia eneo langu niliwatafsiri vibaya nilidhani ni watu wanaopinga maendeleo…lakini cha ajabu wamekuwa msaada mkubwa kuchochea maendeleo na
wakati mwingine hushirikisha wananchi kuleta maendeleo juu ya changamoto za huduma za kijamii, natamani wangesambaa mikoa yote,” alisema Bw. John alipokuwa akichangia.

Diwani Kata ya Mshewe, Ester Mbega alisema uwepo wa vituo vya taarifa na maarifa vinavyo amasishwa na TGNP Mtandao umesaidia sawa kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za miradi ya maendeleo eneo hilo. Aliiomba TGNP Mtandao kuendelea kuwawezesha wanachama wa programu hiyo jambo ambalo litaongeza kasi ya maendeleo kwenye maeneo yao.

“…Binafsi naona uwepo wa vituo vya taarifa na maarifa ulichelewa, wamekuwa wakipambana na vitendo vya unyanyasaji hali ambayo imesaidia kupungua kwa vitendo hivyo eneo letu,” alisema Bi. Mbega.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Nsalala, Kissman Mwangomale aliiomba TGNP Mtandao kuviwezesha vituo hivyo ili kuvijengea uwezo katika kutekeleza majukumu yake, kutokana na

umuhimu vinavyouonesha kuhimiza shughuli za maendeleo kwenye maeneo yao.

Madiwani hao zaidi ya 20, katika mkutano huo pia walipata fursa ya kushirikisha masuala ya

kijinsia, huku wakiangalia namna bajeti za Halmashauri zao zinavyoweza kufanikiwa kutenga

rasilimali za kuhakikisha bajeti zao zinakidhi mahitaji ya kijinsia.