Na Happy Lazaro, JamhuriMedia, Arusha

Arusha .Madiwani wa Baraza la Halmashauri katika Jiji la Arusha wamemuomba Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda agombee ubunge katika Jimbo la Arusha Mjini kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika oktoba mwaka huu 2025.

Madiwani hao akiwemo Naibu Meya wa Jiji la Arusha Abraham Mollel na Diwani wa Kata ya Themi Lobora Petro wakiongea kwenye kikao maalumu cha Madiwani cha kujadili bajeti wamesema kuwa kwa namna Makonda anavyogusa Watu muda ukifika anatakiwa achukue fomu.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Paul Makonda akizungumza katika baraza hilo leo.

“Maneno ya kwenye Biblia yanasema mfalme yeyote ni yule mtu anayetoka kwenye Jamii ndogo sana na huwa anaandaliwa.”

“.Sisi tunasikia na tunakaa na watu, watu wanasema kwa namna unavyogusa maisha ya watu na watu wakisema sauti ya watu ni sauti ya Mungu, ikikupendeza, muda ukifika chukua fomu na sisi tupo nyuma yako. Ingawa tumepangiwa watu ila mimi siogopi kwani kote huku ni Mungu kaniweka. Chukua haya maneno, kaendelee kutafakari, wewe ni muombaji na sisi tutapeleka jina lako madhabauni.” amesema Naibu Meya.

Madiwani hao kwa Nyakati tofauti wamempongeza Makonda kwa uchapakazi wake katika kutimiza maelekezo ya . Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na kusimamia vyema Ilani ya CCM ya mwaka 2020/25, huku Diwani Lobora akiomba radhi kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Arusha Mjini kutokana na madai ya kumpendekeza na kumchagua mtu asiyefaa katika nafasi ya Ubunge mnamo mwaka 2020.

Madiwani wa jiji la Arusha wakiwa katika baraza.
Meya wa jiji la Arusha ,Maximilian Iranghe akiwasalimia madiwani alipowasili kwenye kikao hicho kwa ajili.ya kuanza kikao hicho rasmi .