Na Byarugaba Innocent, JamhuriMedia, Kibaha

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Dkt.Rogers Jacob Shemwelekwa mapema leo Agosti 30, 2024 amekabidhiwa TUZO MAALUM ya uongozi Bora, Upendo na kuwajali watumishi kutoka kwa Madereva 20 wa Magari na Mtambo wanaofanya kazi kwenye Halmashauri ya Mji Kibaha.

Hafla hiyo imefanyika Ofisini kwa Mkurugenzi ambapo Kiongozi wa Madereva hao Fatuma Musaa akiwa sambamba na wenzeka alimkabidhi TUZO hiyo Maalum iliyonakishiwa kwa maneno ya lugha ya Ughaibuni yalisomeka

“With greater Appreciation Dr.Rogers J.Shemwelekwa .Thank you for your steadfast Commitment,for your thoughtful guidance and inspiring leadership present on each of your action.Let our unforgettable gratitude greet you with love for your example,for believing instilling in us”. We are KTC drivers.

Mwenyekiti wa Madereva hao Innocent Nelly ameeleza kuwa kwa Madereva wamewiwa kutoa TUZO hiyo kwa Moyo mweupe kwa sababu kubwa tatu;
Mosi,Madereva na watumishi wa kada nyingine kupewa heshima na Mwajiri huyo kuhudhuria kilele cha maonesho ya Sherehe za Nanenane,2024 kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.

Pili Kuruhusiwa na kugharamiwa kongamano la Madereva nchini lililofanyika kuanzia tarehe 18-24 Agosti,2024 lililohitimishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Majaliwa K. Majaliwa Jijini Arusha na

Tatu kuanza kupewa posho ya kila Mwezi chini ya uongozi wake inayowawezesha hata kugharamia mahitaji madogo madogo ikiwemo kuosha vyombo vya usafiri wanavyoviendesha

Akipokea TUZO hiyo, Dkt.Shemwelekwa amewashukuru sana Madereva hao kwa Moyo wa kutambua na kuthamini kazi wanazozifanya.Aidha, amewaasa Madereva hao kufanyakazi kwa kuzingatia sheria, taratibu, Kanuni na miongozo inayowaongoza.

Aidha,amewasisitiza kuwahi kazini kwani ni takwa la Kisheria, kutunza vyombo vyao, kuwaheshimu viongozi na watumishi wengine wanaowaendesha,kuwa nadhifu mara zote na kufanyakazi kwa upendo na kushirikiana mara zote

Sambamba na hilo Dkt.Shemwelekwa amewaasa kupenda kujiendeleza kielimu ili kujiboresha na kupata maarifa mapya kwa kusoma kozi fupi na kuahidi kuwagharamia kadri Bajeti itakavyoruhusu.

Fatuma Mussa ametoa na neno la shukrani kwa niaba wa wengine amesema kuwa wapo tayari kufanyakazi usiku na Mchana kwa bidii, maarifa na weledi kwa kuzingatia sheria za nchi na kwamba wapo tayari kuwajibika kwa Maslahi mapana ya Kibaha Mji na Taifa kwa ujumla.

Aidha,Fatuma ametumia nafasi hiyo kumkabidhi Dkt. Shemwelekwa Kitabu Maalum kama ishara ya kuandika taarifa mbalimbali za utekelezaji wa kazi zao.

Ikumbukwe kuwa Dkt.Rogers Jacob Shemwelekwa aliteuliwa rasmi Mwezi Machi, 2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha akitokea Shirika la Elimu Kibaha alikokuwa Mkurugenzi wa Huduma za Elimu.