Madatari katika hospitali za umma nchini Nigeria wameanza “mgomo na usio na kikomo” kutokana na kile walichokieleza kuwa ni kushindwa kwa serikali kushughulikia malalamishi yao.

Madaktari wanaogoma ni asilimia kubwa zaidi ya madaktari katika hospitali za Nigeria.

Mgomo wa namna hiyo kwa kawaida huvuruga sana huduma za afya katika hospitali za serikali.

Miongoni mwa madai yao, ni pamoja na malipo ya haraka ya mishahara yote na posho mpya ya hatari.

Chama cha Madaktari cha Nigeria kinasema angalau madaktari 50 huondoka Nigeria kila wiki kwenda kufanya kazi nje ya nchi.

Hali mbaya za kazi, pamoja na malipo mabaya na kupanda kwa gharama ya maisha ni sababu kuu.