Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimfanyia mgonjwa ambaye mshipa mkubwa unaosambaza damu upande wa kushoto wa moyo umeziba upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting).

Madaktari Bingwa wa Usingizi na wagonjwa mahututi wa moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiangalia jinsi moyo wa mgonjwa unavyofanya kazi (mapigo ya moyo) kwa kutumia mashine maalum wakati mgonjwa huyo akifanyiwa upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting).
Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto Godwin Sharau wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Benjamin Bierbach wa nchini Ujerumani wakimfanyia upasuaji wa kuziba matundu ya moyo mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na mwezi mmoja.
Post Views: 219