Serikali ya Madagascar imeidhinisha sheria ya kuhasiwa kwa atakayekutwa na hatia ya ubakaji dhidi ya watoto.

Ni sheria ambayo imezua minongono na mabishano ndani ya Bunge la nchi hiyo.

Mwezi wa pili ndipo bunge la Seneti la Madagascar lilipoipitisha sheria hiyo na kumpelekea Rais Andry Rajoelina kwa ajili ya kuidhinisha.

Kuhasiwa kwa njia ya upasuaji kwa atakayekutwa na hatia ndiyo sheria iliyoidhinishwa baada ya Bunge kupinga njia ya kutumia dawa ambayo inakiuka sheria za nchi.

Licha ya raia wa nchi hiyo kupongeza hatua hiyo ya serikali, Shirika la Kimataifa la kutetea haki za Binadamu Amnesty International limepinga kuidhinishwa kwa sheria likisema kuwa ni ukiukwaji wa haki za Binadamu.

Tangu mwezi Januari mwaka huu vilikuwa visa vya ubakaji zaidi ya mia moja na thelathini wakati mwaka uliopita viliripotiwa visa zaidi ya 600 nchini Madascar.

Please follow and like us:
Pin Share