Na Magrethy Katengu,JamuhuriMedia, Dar es Salaam

Mabalozi wa Nchi za Afrika nchini Tanzania wanatarajia kushiriki mbio za riadha kuanzia kilomita 5 hadi 15 zitakazofanyika Mei 18 ,2024

Ameyasema hayo leo Mei 15, 2024 Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mindi Kasiga katika mkutano wa waandishi wa habari na Umoja wa Mabalozi wa Nchi za Afrika nchini ambapo amebainisha kuwa katika mbio hizo kutakuwa na makundi mawili kundi la kwanza watakimbia kilomita tano na kundi lingine watakimbia kilomita 15 .

Hata hivyo amebainisha kuwa mbio hizo zitaanzia Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere- Dar es Salaam, kuanzia majira ya saa 12 asubuhi kwa kuanza na kundi la kwanza litalokimbia kilomita 15, kupitia barabara ya Baraka Obama na kuelekea hadi Aga khan na kupita daraja la Tanzanite hadi Masaki na hatimae kugeuza na kurudi JINCC.

Sambamba na kundi la pili watakimbia kilomita tano wataanza saa 12:30asubuhi asubuhi na capital barabara Baraka Obama na kukimbia hadii Aghakhan hospitali kisha kurudia Ukumbi wa JINCC.

“ Katika riadha hii tumewalika wakimbiaji mashughuli kutoka Tanzania ili kuadhimisha siku hii, ambao wengine ni wakimbiaji walioshinda kwenye mashindano ya riadha ya Olimpiki na tayari wamejisajili ,”alisema.

Balozi Mindi amefafanua kuwa maadhimisho hayo yanafanyika kila mwaka Mei 25 ambapo kwa mwaka huu watafanya kwa kushirikiana na kundi la mabalozi wa Afrika, hivyo wameona waadhimishe siku hiyo kwa mbio za riadhaa kwa ajili ya kusherekea Siku ya Afrika.

Aidha riadha hiyo itakuwa sio ya kawaida watu watalipa hela na watajiandikisha lengo ni kukusanya fedha kwa ajili ya kwenda kusaidia shule za wanafunzi wenye mahitaji maalum zilizopo jijini Dar es Salaam hivyo kitakachopatikana kutokana na riadha hizo basi kitaenda katika hizo shule.

Aidha wanariadha wa Kitanzania ambao wameweka alama kimataifa, Juma Ikangaa, Alphonce Simbu, Filberty Bayi na wengineo watarajia kuwemo katika mbio ambazo zimepewa jina la Africa Day Marathon zinazotarajiwa kufanyika Mei, 18 mwaka huu jijini Dar es Salaam.


Mbio hizo ni maalumu kwa ajili ya mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini hususan waafrika kukimbia ikiwa ni kukumbuka kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika (OAU) Mei 25, 1963, Adisababa nchini Ethiopia uliokuwa na lengo la kuzikomboa nchi ambazo hazikuwa huru kwa wakati huo.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Mashariki Wizara ya Mambo ya Nje,Balozi Bujiku amesema mbio hizo maalumu ni kwa ajili ya kuadhimisha miaka 61 ya kuanzishwa OAU mwaka 1963 na mwaka 2002 kubadilishwa jina na kuitwa (AU) baada ya nchi zote za Afrika kuwa huru na sasa wakiwa wanaangalia mafanikio na kupanga mikakati ya kusonga mbele na kujiletea mafanikio katika nyanja mbalimbali.

“Nchi nyingi za Afrika zinaadhimisha siku hiyo Mei, 25 kila mwaka, kwa Tanzania tunaadhimisha Mei 20, kutokana na Mei 25, 2024 kutakuwa na ugeni wa Baraza la Amani na Usalama,” amesema.

Pia amesongeza kuwa baada ya mbio hizo, watapeleka misaada katika shule zenye wahitaji maalumu nne, mbili zikiwa za Shule za Msingi na mbili za Sekondari ambazo ni Jangwani, Pungu, Uhuru Mchanganyiko na Jeshi la Wakovu.