Na Mwamvua Mwinyi,JamhuriMedia,Kibaha
Halmashauri ya Mji Kibaha,imeendesha semina ya kuwajengea uwezo maafisa Elimu kata,walimu walimu wa shule za msingi na sekondari juu ya masuala ya VVU/UKIMWI mahala pa kazi kwa lengo la kuondoa unyanyapaa na ukatili wa kijinsia.
Siwema Cheru ni Mratibu wa UKIMWI wa Halmashauri ya Mji Kibaha amesema semina hiyo ni mwendelezo wa Mafunzo mengine ambayo yamekuwa yakitolewa kwa wadau mbalimbali ili kuondoa vitendo vya unyanyasaji sehemu za kazi na kwamba sasa wamefikiwa waratibu wa Elimu kata na walimu ambao ni wadau wakubwa kwenye jamii na wanakaa na wanafunzi muda mrefu ambao pia ni wahanga
Dr.Mariam Ngaja ameeleza , walimu wakipata uelewa wa semina hiyo wanawajibu wa kuwafundisha wanafunzi wao kuhusu afya ya uzazi kwa Vijana na maradhi yanayoambukizwa kwa njia ya ngono na Elimu ya madawa ya kulevya.
Ngaja ameongeza , semina hiyo ambayo ni utekezaji wa kawaida wa idara ni utekelezaji wa mkakati wa nne wa Taifa wa kudhibiti UKIMWI Tanzania hasa kwa wasichana balehe na wanawake vijana .
Mwalimu Augustine Seso aliyeshiriki semina hiyo aliishukuru Halmashauri na kueleza imewafikia muda muafaka na sasa wanakwenda kwenye jamii kutimiza lengo la kutoe elimu ili kuondosha unyanyasaji na ukatili wa kijinsia kwenye jamii.