Na Mussa Augustine,JamhuriMedia

Diwani wa Kata ya Mzimuni Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Manfred Lyoto ameanzisha Taasisi ijulikanayo kama Lyoto Development Foundation ili kuhakikisha inatoa mikopo isiyokuwa na riba kwa wananchi wa kata hiyo ili wafanye shughuli za kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza na JAMHURI MEDIA Diwani Lyoto amesema kuwa taasisi hiyo imeanzishwa kutokana na fedha zinazotolewa na halmashauri kwa ajili ya mikopo kwa makundi ya Vijana,Wakina mama na Watu wenye ulemavu kushindwa kujitoshereza kutokana na mahitaji ya mikopo kuwa makubwa huku fedha zikiwa kidogo.

Amesema kuwa taasisi hiyo tayari imesajiliwa ipo chini ya usimamizi wa ofisi yake nakwamba itaanza kutoa mikopo hiyo muda siyo mrefu kwa wananchi ili kuisaidia halmashauri katika kutoa mikopo kwa wananchi nakuwafanya wajishughulishe katika biashara ndogondogo nakujikwamua kiuchumi.

“Taasisi ya Lyoto Development hivi karibuni itaanza kutoa mikopo bila riba kwa wananchi wa kata hii,halmashauri ina mambo mengi yakufanya hivyo fedha inazotenga hazitoshi kwani watu wengi wanataka mkopo,kupitia taasisi hii tutakua tuawapa mkopo wale wanaokosa kule halmashauri wakija hapa tunawapa ,lengo langu ni kuwainua kiuchumi wananchi wangu”amesema Diwani Lyoto
Nakuongeza kuwa ;

“Taasisi hii nimeanzisha mwenyewe kupitia vyanzo vyangu vya kipato na pia nimepata mfadhili ambaye tupo katika hatua za mwisho ili tuanze kutekeleza yale tuliyokusudia,nachokiomba wananchi wenye uwezo wa kiuchumi wajitolee kuwasaidia wananchi ambao hawana uwezo kiuchumi.

Kuhusu taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kata ya Mzimuni Diwani Lyoto amesema kuwa sekta ya elimu na afya amezipa kipaumbele zaidi ambapo tayara baadhi ya changamoto amezipatia ufumbuzi ambapo Sekta ya Elimu amefanikwa kujenga uzio unaozunguka shule ya Sekondari Mzimuni,Shule ya Msingi Mzimuni na Mikumi ambapo ujenzi huo umekamilika nakuweza kuondoa adha walizokuwa wakukumbana nazo wanafunzi wanaosoma shuleni hapo.

Aidha Diwani Lyoto amesema kuwa amefanikiwa pia kufanya ukarabaiti wa madarasa kwenye shule za msingi Mzimuni na Mikumi,pamoja na kununua mashine ya kuchapishia mitihani(photocopy Machine) ambayo inauwezo mkubwa hivyo inatumiwa na shule zote tatu za Sekondari Mzimuni Shule ya Msingi Mzimuni na Mikumi,nakwama mashine hiyo imegharimu kiasi cha shilingi milioni 3.

Ameendelea kusema kuwa katika shule hizo pia amenunua kontena lenye gharama ya kiasi cha shilingi milioni 7.5 ili kutumika kwa ajili ya kuhifadhia chakula na kuwepo kwa ofisi ya kuratibu chakula kwa wanafunzi wa shule hizo,pamoja na kutumia shilingi milioni 1.5 kukarabati jiko,huku milioni 2 zikitumika kununua vifaa vya jiko,ambapo tayari wanafunzi wameanza kupata chakula cha mchana shuleni hapo.

Amesema kuwa ameajiri walimu wa masomo ya sayansi ambapo amekuwa akiwalipa posho kila mwisho wa mwezi hali ambayo imechangia shule ya Sekondari Mzimuni kupata wanafunzi sita wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza(Devision one),ambapo pia amekuwa akitoa motisha kwa walimu na wanafunzi wanaofanya vizuri ikiwa lengo ni kuhamasiha kukuza ufaulu katika shule hizo.

Akizungumzia kuhusu sekta ya afya amesema kuwa zahanati ya Kata ya Mzimuni ilikuwa na changamoto kubwa ya upungufu wa watumishi,lakini katika uongozi wake wa miaka miwili tangu 2022 alipochaguliwa kuwa diwani wa kata hiyo ameleta watumishi watatu ambao ni daktari mmoj,Nesi mmoj,na Mtaalamu wa Maabara mmoja ambapo amekuwa akiwapa fedha yake mwenyewe shilingi milioni moja kila mwezi kama posho ambapo kwasasa wananchi wanapata huduma kwa wakati tofauti na hapo awali watumishi waliku wawili tu.

Kuhusu Miundombinu ya barabara amesema kuwa tayari barabara ya kutoka Magomeni Mapipa hadi Mabibo yenye urefu wa kilometa 8,imekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami na imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 17,huku barabara ya Dick Sound ambayo imekua kero ya muda mrefu kwa wananchi wa eneo hilo imeshafanyiwa marekebisho.