Na Isri Mohamed, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mjumbe wa bodi ya wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mzee Azavel Lwaitama amewataka wanachama cha Chama hicho kuzingatia umoja wao hasa baada ya uchaguzi kumalizika, kwani migogoro ya ndani inaweza kusababisha chama Chao kifutike katika tasiwra ya siasa nchini.

Mzee Lwaitama ameyasema hayo katika ukumbi wa Ubungo Plaza kwenye uchaguzi wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) ambapo amewataka watakaoshinda kujiepusha na ulevi wa ushindi, na kutumikia watu wote hata wale ambao hawakuwachagua.

Mkutano mkuu wa BAWACHA utakaoambatana na uchaguzi mkuu umefunguliwa leo Januari 16, na Mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Mbowe.

Uchaguzi umeanza kufanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam na unatarajia kutamatika kesho.