Na Mwandishi wetu JAMHURI MEDIA

Lori linalosafirisha Mafuta limepata ajali na kuwaka moto mkubwa katika maeneo ya Ubungo jirani na Kituo cha Mabasi yaendayo Kasi cha Kibo barabara ya morogoro, jijini Dares Salaam.

Jeshi la Zimamoto limefika eneo la tukio na linaendelea na zoezi la kuzima moto huo.

Hadi sasa bado haijafahamika madhara kamili yaliyopatikana kutokana na Ajali hiyo ingawa taarifa za awali zinaeleza kuwa baadhi ya Nyumba za jirani na Pikipiki 2 zimeteketea kwa Moto huo.

Please follow and like us:
Pin Share