Liverpool imewazuia Manchester City katika jitihada zao za kumaliza msimu wa Ligi ya Uingereza bila kupoteza mchezo

Jurgen Klopp amesimamisha utawala wa Pep Gurdiola Premier League, baada ya michezo 30 bila kupoteza mechi hata moja hatimaye hii leo Liverpool wamefanikiwa kuipiga Manchester City bao 4 kwa 3.

Ni Arsenal Mae 2003 hadi Oktoba 2004 na Chelsea Mei2013 hadi Oktoba 2014 (Mechi 40), ndio ambao wamecheza mechi nyingi zaidi bila kupoteza kuliko rekodi hii ya City iliyodumu kuanzia Aprili mwaka jana.

Baada ya matokeo ya leo sasa Liverpool wanakuwa wanaendeleza rekodi yao ya kutofungwa na Manchester City katika uwanja wao wa nyumbani na kufikia mechi 15, idadi kubwa zaidi kwa City kutopata ushindi kwa timh moja ugenini.

Kabla ya hapo Arsenal walipoteza mchezo dhidi ya FC Bournamouth, mchezo wa leo ilikuwa mechi ya kwanza kwa Bournemouth kuipiga Arsenal katika michezo yao 6 iliyopita na hii ikiwa mara ya kwanza kwa Bournemouth kupata alama mbele ya timu top 6.

Kwa matokeo ya leo msimamo wa ligi umebadilika katika nafasi nne za juu ambapo sasa Liverpool wamepanda hadi nafasi ya tatu ya msimamo huo wakiwa na alama 47 huku wakiwazidi Chelsea kwa tofauti ya mabao.