Ligi kuu nchini uingereza iliendelea tena jana kwa mechi kazaa ambapo liverpool imeitandika Swansea City kwa magori 5-o, magaori hayo yalifungwa na Roberto Firmino
ambaye alifunga magori mawili dakika 52 na 66 , magoli mengine yalifungwa na Trent Alexander-Arnold alifunga dakika 65, na Alex Oxlade-Chamberlain alifunga dakika 82. Mechi nyingine ilikuwa kati ya Tottenham Hotspur dhidi ya Southampton ambapo katika mechi hiyo Tottenham Hotspur iliibuka na ushindi wa mabao 5-2 mabao ya Tottenham Hotspur yalifungwa na Harry Kane ambaye alifunga magori matatu dakika 22, 39 na 67 , magoli mengine yalifungwa na Dele Alli alifunga dakika 49, Heung-Min Son alifunga dakika 51 huku magoli ya Southampton yalifungwa na Sofiane Boufal dakika 67 na laipili lilifungwa na Dusan Tadic dakika 82.
Mbali na Michezo hiyo pia kulikuwa na mechi kati ya Manchester United dhidi ya Burnely ambapo katika mchezo huo timu zote mbili zilitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2, mabao yote ya Manchester yalifungwa na Jesse Lingard, na mabao ya Burnley yalifungwa na Ashley Barnes pamoja na Steven Defour.
Matokeo za mechi zingine

AFC Bournemouth 3 – 3 West Ham United

Chelsea 2 – 0 Brighton & Hove Albion

Huddersfield Town 1 – 1 Stoke City

Watford 2 – 1 Leicester City

West Bromwich Albion 0 – 0 Everton