Leo June 13 ni siku ya Uelewa wa watu wenye Ualbino Duniani ambapo kwa Tanzania kitaifa inafanyika mkoani Simiyu.
Pamoja na kampeni mbalimbali jamii ya watu wenye ulemavu wa ngozi bado inaishi kwa mashaka kutokana vitendo vya imani potofu ambavyo vinaendelea kuripotiwa maeneo mbalimbali vikilenga watu wa jamii hiyo.
Watu wenye ulemavu kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa upendo kutoka kwa baadhi ya watu wenye imani potofu wanaowauwa au kuwasababishia ulemavu kwa ajili ya kuhitaji viungo vyao.
Kilio kikubwa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi ni usawa, haki ambayo kwa wenzetu wenye ulemavu wa ngozi wamekuwa wakililia kwa muda mrefu kutokana na mazingira wanayoishi.
maadhimisho hayo yanakwenda sambamba na kauli mbiu isemayo, ‘’ tunaangaza mwanga wetu duniani
‘’ shining our light world”.