Na Isri Mohamed, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema, ameweka wazi kuwa kuna watu walienda kwa mama yake mzazi kumtaka azungumze nae ili amuunge mkono kaka yake Freeman Mbowe katika uchaguzi wao mkuu unaotarajiwa kufanyia Januari 21, 2025.
Lema amesema watu hao walimueleza mama yake kuwa endapo atamuunga mkono Lissu, na Mbowe akashinda kwenye uchaguzi basi atapoteza nafasi ya kugombea ubunge Arusha mjini.
“Nataka kuwatoa hofu watu hao kwamba sitagombania ubunge Arusha mjini kwa mwaka 2025, sifanyi harakati ili nipate ubunge, ila atakayegombania nitamsaidia kuongea na rasilimali” amesema.