*Kuna ongezeko la leseni zitolewazo kwa madereva.
*Kuanza kwa safari za saa 24 kumeketa mafnikio, wengi wasafiri usiku
*Uimarishwaji wa miundombinu ya barabara.
Na Lookman Miraji
Mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa ardhini nchini LATRA imeelezea tathmini ya mafanikio ya uendeshaji wake chini ya serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari, Mkurugenzi Mtendaji wa LATRA, CPA: Habibu Suluo amesema kuwa mamlaka hiyo imepiga hatua kubwa katika baadhi maeneo hususani katika nyanja hiyo ya usafishaji.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo imeeleza kuhusu ongezeko la leseni zitolewazo kwa madereva waliosajiwa ikiwa sehemu kubwa ya kuchochea unafuu wa uhaba wa madereva wenye kuzijua vyema sheria za barabarani.
Idadi ya jumla ya leseni zaidi ya laki tatu zimetolewa kwa madereva wa vyombo vya moto nchini.
Ripoti hiyo iliyotolewa leo hii na CPA: Habibu Suluo imeyaelezea mafanikio ya kuanza kwa safari za saa 24 , sehemu inayotajwa kama hatua muhimu katika kurahisisha usafirishaji.
Mfumo huo wa safari za mikoani kwa saa 24 ulianza kutumika rasmi mwezi Oktoba mwaka 2023 mara baada ya zuio la safari hizo lililowekwa mwaka 1994 .
Aidha ripoti hiyo pia imepongeza jitihada za serikali kupitia Wizara ya ujenzi kwa kusaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha miundombinu ya barabara zitumikazo katika shughuli mbalimbali.
Baadhi ya barabara hizo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kuepusha msongamano mkubwa wa magari ambao huweza kusababisha ajali ambazo husababisha maelfu ya watanzania kupoteza maisha.
Ripoti hiyo imetolewa leo hii mbele ya wahariri wa vyombo vya habari pamoja na viongozi wengine wa mashirika ya usafirishaji.