……………………………………………….

Zaidi ya watu laki tano wamepata huduma ya ushauri nasaha na kupima maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kupitia mradi wa CDC/ PEPFA afya hatua katika kipindi cha kuanzia Oktoba 2022 hadi Disemba 2023.
Akizungumza wakati ya Kilele cha wiki ya vijana kwenye maadhimisho ya UKIMWI Duniani ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Morogoro, Mkurugenzi wa Miradi shirika la Tanzania Heath Promotion Support (THPS) Dkt.Eva Matiko amesema kati ya watu hao waliopima zaidi ya 5000 asilimia 3.2 takribani watu 16231 wamegundulika kuwa na maambukizi ya VVU na 141197 wapo kwenye huduma ya matunzo kwa WAVIU huku asilimia 98 wana umri zaidi ya miaka 20.
Amesema kupitia mradi wa Global Fund Malango II wamefanikiwa kuwafikia watu walio katika mazingira hatarishi 21289, miongoni mwao 17665 walipata huduma ya kupima VVU ambapo asilimia 12 waligudulika kuwa na VVU na asilimia 94 walianzishwa dawa za kufubaza virusi ( ART).
Vaileth Kalovela mkazi wa Kibaha mkoani wa Pwani ni moja wa wanufaika wa mradi wa CDC/ PEPFA amesema mradi huo umeweza kumlea tangu akiwa na mri mdogo mpaka sasa anamiaka 24 akiwa mke na mama mtalajiwa.
Anasema kupitia huduma rafiki ambazo zinatolewa na mradi wa CDC/ PEPFA kwa watoto na vijana zimemfanya kuweza kuwa na afya njema kwa kuzingatia matumizi ya dawa za kufubaza VVU na kukua kiakili, kujitambua na kuchangamana na watu wengine hali inayofanya kujiona yupo sawa na watu wengine.
“Kupitia Camp za vijana za CDC/ PEPFA niliweza kukutana na mwenza wangu na mpaka sasa tunatarajia kupata mtoto siku za karibuni”.Alisema Vaileth Kalovela nmnufaika wa mardi wa CDC/ PEPFA.
Tanzania Heath Promotion Support THPS ni Taasisi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa mwaka 2011 inayotekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa OR-TAMISEMI, Wizara ya Mambo ya ndani na Wizara ya afya Zanzibar.