Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi – Dar es Salaam
Jeshi la Polisi kupitia Kamisheni ya Polisi Jamii Dawati la Ushirikishwaji wa jamii Makao Makuu ya Jeshi la Polisi imetoa mafunzo kwa kundi la maofisa na Wakaguzi Wasaidizi wa Polisi wanafunzi kutoka chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) namna ya kushirikisha jamii katika kubaini, kuzia na kutanzua uhalifu hapa nchini.
Akitoa mafunzo hayo Mrakibu wa Polisi SP Dr.Ezekiel Kyogo kutoka kamisheni ya Polisi Jamii dawati la Ushirikishwaji wa jamii Makao Makuu ya Jeshi la Polisi amesema maafisa hao wanaowajibu wa kisheria wa kulinda rai ana mali zao huku akibainisha kuwa zipo taratibu za kishera katika maswala ya kiulinzi na kuwashirikisha wananchi ambapo amewataka askari hao kuwaelewesha wananchi dhana dhima ya ushirikishaji jamii kiundani ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa dhana ya Polisi Jamii.
Dk. Kyogo pia amewaeleza maafisa hao kuwa wakifuata misingi ya ushirikishwaji jamii kikamilifu itawasaidia katika utendaji wa kazi za Jeshi la Polisi na wananchi watashiriki kikamilifu katika maswala ya ulinzi huku akibainsha kuwa dira ya Jeshi hilo ni kutoa huduma bora na nzuri kwa wananchi ambapo amewataka askari hao kutoa huduma bora kwa wananchi ili kupunguza malalamiko yanayotolewa.
Amesisitiza kuwa askari wanaowajibu kuwapa elimu wananchi juu ya ushiriki wao katika ulinzi ili kudhibiti vitendo vya uhalifu katika jamii pia amewataka askari hao kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wa Jeshi la Polisi kwa kutoa huduma bora ambazo wananchi watazifurahia.
Amewataka maofisa hao wanafunzi na wakaguzi wasaidizi wa Polisi mara baada ya kumaliza mafunzo yao na kupangiwa kazi na Mkuu wa Jeshi ls Polisi nchini wakatende haki na kutoa huduma bora kwa wananchi huku akibainisha kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wamepunguza malalamiko Juu ya Jeshi hilo.