Na Isri Mohamed, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Baraza la vijana la chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) taifa, Wakili Deogratius Mahinyila, amekiri kuwa uchaguzi wa baraza lao ulitawaliwa na rushwa.
Wakili Mahinyila ameyasema hayo wakati akitoa wito kwa vijana wa Chadema nchi nzima kusafiri kuja jijini Dar es Salaam kushiriki katika mkutano wao na uchaguzi wao mkuu unaotarajia kufanyika Januari 21, 2025.
Aidha Wakili Mahinyila amekemea vitendo hivyo vya rushwa na kuwataka wanachama hasa vijana kuhakikisha uchaguz huo unakuwa na huru na haki.
Katika hatua nyingine, Wakili Mahinyila ameonesha kuchukizwa na kauli zinazoashiria kuwa kuna mipango kwa baadhi ya wanachama kuhama Chadema kwenda vyama vingine baada ya uchaguzi, Pale tu wagombea wao watakaposhindwa.