Na Adeladius Makwega-Buigiri
Wakristo wameambiwa kuwa Kipindi cha Kwaresma ni cha kusali zaidi, kipindi cha kuombeana mbele za Mungu na kipindi cha kujikadihi kwa Mwenyezi Mungu.
Hayo yamesemwa an Padri Paul Mapalala Parokiani Chamwino Ikulu katika Kanisa la Bikira Maria Imakulata, Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma katika misa Jumapili ya Pili ya Kwaresma Machi 5, 2023.
“Kristo amekuja duniani kutukomboa na kutuokoa, inategenea kila mmoja uwazi wake na utayari wake, kuwa na Kristo pamoja, atakapo kubali kuwa na Kristo katika kipindi chote na kwa kufanya hivyo ni kuzidi kumuelewa Mwenyezi Mungu yeye nani ,nani mwokozi na mkombozi wetu, na nani mwezetu tunayeaye? Kwaresma ni kipindi cha kutambua kuwa kila mmoja anayo mahitaji yake mbele ya Mungu hakuna aliyekamilika”
Misa hiyo pia iliambatana na maombi kadhaa na mojawpao lilikuwa hili.
“Uwashirikishe marehemu wetu utukufu wako.”Kwa ujumla hali ya hewa ya eneo la Chamwino Ikulu kwa juma hili mvua imenyesha mara mbili ambapo kidogo inaweza kuyasaidia mahindi ambayo hayajatoa mbelewele lakini wakulima wengi wanasema kuwa mahindi yaliyokwisha toa mbelewa hayawezi kuweka chochote hata kama yatakuwa hai yanaweza kuwa na mabunzi yenye punje chache sababu ikiwa kukosesekana mvua ya kuitosha.