Na Mwandishi wetu.
Wakala wa Djuma Shaaban na Yanick Bangala ameshusha chuma kingine Tanzania. Straika mcongo, Jean Baleke Othos (21), yupo chini ya menejimenti ya faustyworld ambaye ni wakala wa Djuma Shaaban, Yanick Bangala wa Yanga na Ben Malango.
Ujio wa Jean Baleke aliyekuwa akikipiga TP Mazembe kabla ya kutimkia Nejmeh ya Lebanon ambako alicheza mechi 11 na kufunga magoli 3 unaipa Simba ya Ribertinho sura mpya kabisa katika eneo la ushambuliaji.
Simba ya kibrazil itajipanga katika kikosi chenye viungo wengi zaidi watakaokuwa na kazi ya kumlisha Baleke pasi za magoli. Simba inaweza kuanza na Manula golini, beki ya kulia Shomari Kapombe, kushoto Zimbwe Jr, beki za kati ni Henock Inonga Baka ambapo hakutakuwa na mabadiliko ya mara kwa mara katika eneo hilo la ulinzi.
Eneo la kiungo ambapo akili ya Robertinho ndipo hukaa inaweza kuwa na Sawadogo na Sadio Kanoute kama double Pivot halafu kulia anacheza Chama na kushoto Pape Osman Sakho huku namba kumi akicheza Saido Ntibanzokiza na namba tisa Baleke mwenyewe.
Mwalimu Robertinho atakuwa na nafasi ya kumuweka Sawadogo na Mzamiru kama double Pivot halafu juu yao akakaa Moses Phiri halafu kushoto na kulia wakacheza Chama na Augustine Okrah ili kumlisha pasi na krosi Baleke wakati huo Saido na Sadio Kanoute wakiwa wanasubiria benchi.
Upana wa kikosi cha Simba utaanzia hapo kwa sababu unapoanza na mafundi wengi namna hiyo bado nje ya uwanja kuna Bocco, Kakolanya, Mwenda, Kennedy Juma, Nungunungu, Kibu, Kyombo na wengine wenye uwezo wa kuifanyia timu makubwa. Na hii ndio Simba itakayowafanya wapinzani maji waite mma.