Orodha ya kila mwaka ya viwango vya furaha inaendelea kuongozwa na nchi za Nordic, zinazozijumuisha Denmark, Finland, Iceland, Norway na Sweden, huku Finland ikiendelea kushikilia nafasi ya kwanza miongoni mwao tangu mwaka 2018. Denmark ni ya pili, Iceland (3), Sweden (4) na Norway ya 7.

Viwango vya furaha vya nchi kupitia maeneo matatu ya ukarimu ambayo ni utoaji wa misaada, kujitolea na kusaidia wageni vilifuatiliwa na kuonyesha kutofautiana sana na vikileta tofauti kubwa ya matokeo kutokana na tofauti za kitamaduni na mifumo ya taasisi.

Nchi za ukanda huu wa Nordic, kama Finland zina furaha zaidi kwa sababu zina mfumo mzuri wa usaidizi wa kijamii kwa sababu wananchi wake wana uhakika wa huduma za afya, elimu na fursa za kiuchumi.

Tanzania inashika nafasi ya chini kwa sababu mazingira yake ya sasa hayawezeshi vigezo vya furaha kupanda.