Mada hii ilitayarishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Othman Masoud Othman, na kuwasilishwa katika Mkutano Maalumu ulioandaliwa na Zanzibar Law Society Kuadhimisha Miaka 41 ya Muungano. Ulifanyika katika Hoteli ya Bwawani, Zanzibar mnamo Aprili 23, 2005. Ukisoma aya moja baada ya nyingine, utaona tofauti ndogo mno katika misimamo ya Uamsho na SMZ. Lililo wazi ni kwamba Muungano unakabiliwa na kifo. Endelea…
“Kinachojidhihirisha ni kuwa tatizo sio la idadi ya Serikali tu, lakini ni zaidi ya hapo. Tatizo la msingi ni lile la Kanuni za msingi za Muungano kutozingatiwa na kutopatiwa majibu. Kutokana na Kasoro hizo ndiyo maana Muungano wetu kama ulivyo hivi sasa hauwezi kuhimili mabadiliko ya kisiasa.”

“Hakuna Muungano madhubuti ambao unategemea kulindwa na sera za chama. Muungano madhubuti ni ule unaolindwa na misingi madhubuti, uwazi na wenye majibu kwa maswali yanayohusu nguzo kuu za Muungano huo.”