Klabu ya Pistons inayoshiriki kwenye Ligi ya Kikapu ya Marekani maarufu kama NBA, imemtema rasmi mchezaji Mtanzania, Hasheem Thabeet, pamoja na nyota wengine wanne.

Maswali yanaibuka kwa kasi juu ya mchezaji huyo kutemwa, ikiwa amecheza mwezi mmoja tu katika klabu hiyo mpya huku wengi wakisema kwamba ni kushuka kwa kiwango.

Thabeet alisaini mkataba usio na hakikisho (a non-guaranteed deal) na Detroit Pistons Septemba 24, baada ya kuachwa na Philadelphia 76ers, ambao walimchukua kutoka Oklahoma City Thunder Agosti 26, mwaka huu.

Thabeet, ambaye alishika namba 2 katika msimamo wa NBA mwaka 2009, alisajiliwa mara moja na Memphis Grizzlies. Wachezaji wengine ambao wametemwa pamoja na nyota huyo wiki iliyopita ni Brian Cook, Lorenzo Brown na Josh Bostic. Mpaka anatemwa alikuwa na rekodi ya kucheza dakika 5 tu katika mechi za kabla ya msimu huu.

Alicheza mechi 23 katika mechi 82, akiwa zote anaingia kutokea benchi, akiwa na uwiano wa pointi 1.2 na 1.7 kufunga karibu na kikapu kwa kasi ya dakika 8.3 kwa mchezo.